Basi la abiria kampuni
ya New Force limegongana na basi dogo la abiria aina ya hiace na kupelekea vifo
vya watu watano na kujeruhi watu wengine tisa, ajali hiyo imetokea leo Machi 4,
2018 majira ya saa nne asubuhi.
Basi la New Force lilikuwa linatokea
Msamvu kwenda Mikese liligongana na gari dogo la abiria (Hiace) lililokuwa
linatokea Msamvu, mkoani Mogororo.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Morogoro,
Urich Matei amethibitisha kutokea kwa ajali hiyo na kusema kuwa watu watano
wamefariki dunia huku wengine 9 wakiwa wamejuruhiwa na wanaendelea kupatiwa
matibabu katika hospitali ya Morogoro.
Kwa mujibu wa mashahuda wa tukio
hilo wamedai kuwa chanzo cha ajali hiyo ni dereva wa hiace ambaye alikuwa
akitaka kulipita gari la mchanga lililokuwa mbele yake hivyo akajikuta amegongana
uso kwa uso na basi hilo.
WATU 5 WAFARIKI DUNIA NA 9 KUJERUHIWA BAADA YA BASI LA NEW FORCE KUGONGANA USO KWA USO NA HIACE
Reviewed by KUSAGANEWS
on
March 04, 2018
Rating:
No comments:
Post a Comment