Shirika hilo
limeeleza kuwa takriban ndoa za utotoni Milioni 25 zimezuiwa
katika kipindi cha miaka 10 iliyopita ambapo kwa sasa mtoto mmoja kati ya
watano wanaolewa kabla ya umri wa miaka 18 ukilinganisha na mmoja kati ya wanne
aliyekuwa anaolewa kipindi hicho.
Nchi za kusini mwa Bara la Asia pia zimepunguza ndoa za utotoni huku
Afrika ikiendelea pia kujitahidi kukabiliana na tatizo hilo ambapo kwa nchi
kama Ethiopia imepunguza tatizo hilo kwa theluthi.
Ripoti hiyo inaeleza kuwa mzigo
wa ndoa za utotoni unaendelea kuzilemea nchi za Kusini mwa Jangwa la Sahara, ambako jitihada zaidi
zinahitajika ili kuondoa tatizo hilo kabisa.
UNICEF inasema
kuwa mmoja kati ya watoto watatu wanapitia ndoa za utotoni kwa kipindi hiki
Afrika ukilinganisha na mmoja kati ya watoto watano waliokuwa wakiolewa miaka
kumi iliyopita.
Viongozi wa dunia wameapa
kumaliza tatizo la ndoa za utotoni ifikapo mwaka 2030 chini ya Malengo Endelevu ya Umoja wa Mataifa (SDGs).
Shirika la Watoto UNICEF latoa Ripoti kuhusu Mimba za utotoni.
Reviewed by KUSAGANEWS
on
March 06, 2018
Rating:
Reviewed by KUSAGANEWS
on
March 06, 2018
Rating:


No comments:
Post a Comment