Katibu wa Itikadi na
Uenezi wa CCM Taifa, Humphrey Polepole, ametoboa siri ya CCM kushindwa mara
mbili mfululizo uchaguzi Jimbo la Mbeya Mjini ambalo linaongozwa na Joseph
Mbilinyi ‘Sugu’ na kusema kwamba Ubaguzi ndiyo chanzo cha mambo yote.
Polepole amesema hayo alipokuwa
akizungumza na viongozi wa CCM ngazi mbalimbali wilaya ya Mbeya Mjini, ambapo
amefafanua kwamba siasa za makundi na ubaguzi wa kikabila zimekuwa zikiikosesha
CCM ushindi kwenye jimbo hilo la Mbeya.
Kiongozi huyo ameongeza kwamba
tatizo hilo lilibainika wakati uongozi wa juu ulipofanya tathmini ya majimbo
ambayo CCM haikushinda kwenye Uchaguzi Mkuu wa 2015, likiwamo jimbo hilo ambalo
ni ngome ya CHADEMA pia yenye madiwani wengi.
Amefafanua kuwa ubaguzi huo umekuwa
ukiifanya CCM kuonekana nyonge/dhaifu mbele ya wapinzani na hivyo kukosa
hoja kwenye uchaguzi pamoja na kuwapa faida wapinzani.
“Siasa za ubaguzi wa kikabila
haziwezi kutufikisha popote, haijalishi kiongozi huyo anatoka kabila
gani, cha msingi awe anashughulikia changamoto za wananchi. Viongozi
fanyeni kila linalowezekana kuondoa tatizo hilo, ili tushinde kwenye chaguzi
zijazo" .
Polepole amesema ubaguzi wa aina
hiyo ni wa miaka mingi hivyo akawataka viongozi wa chama hicho kuhakikisha
wanaondoa changamoto hiyo haraka, ili kufanikisha ushindi kwenye uchaguzi wa
serikali za mitaa mwakani na Uchaguzi Mkuu wa 2020.
POLEPOLE ATAJA SABABU ZA SUGU KUSHINDA MARA MBILI JIMBO LA MBEYA MJINI
Reviewed by KUSAGANEWS
on
March 02, 2018
Rating:
No comments:
Post a Comment