Kaimu Meneja wa Takwimu za Mazingira kutoka Ofisi ya Taifa ya Takwimu Bi.Ruth Minja(Katikati) akiwasilisha Salamu za Taasisi hiyo kabla ya kuwasilisha Takwimu za Utoaji wa huduma za Afya ya Msingi. |
Baadhi ya Wakurugenzi wa OR-TAMISEMI wakifuatilia uwasilishaji wa Takwimu za Utoaji wa huduma za Afya ya Msingi kwa Mama na Mtoto. |
Mkurugenzi Msaidizi wa Utawala Ndg.Mrisho Mrisho
akichangia hoja wakati wa Kikao cha Uwasilishaji wa Takwimu za Utoaji wa huduma
za Afya ya Msingi.
|
Angela Msimbira, OR-TAMISEMI.
Ofisi ya Rais Tawala
za Mikoa na Serikali za Mitaa kuanzia
mwaka 2015-2018 imetekeleza kwa kiasi kikubwa matokeo ya tafiti iliyofanywa na Ofisi ya Taifa ya Takwimu “NBS” kupitia Jukwaa la kukusanya na kuchambua Takwimu za Afya na Lishe “NEP”
iliyofanyika Mwaka 2005-2015.
Akizungumza katika
ufunguzi wa Kikao cha kuwasilisha taarifa hiyo Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais
Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa
Mhe.Selemani Jafo amesema matokeo hayo yamejikita katika Mpango kazi wa Wizara
hii tangu Serikali ya Awamu ya tano ilivyoingia madarakani.
Aliendelea kusema
katika eneo la Miundimbinu ya Afya ambayo imeonekana katika Tafiti kuwa
haikithi mahitaji ya wananchi kwa kutokuwa na huduma muhimu kama vile kuwa na
Wodi za Mama na Mtoto, huduma za upasuaji na sambamba na uhaba wa wataalamu wa
Afya ambapo kwa sasa Wizara inaendelea na maboresho makubwa katika Sekta ya
Afya kwa ujumla wake.
“ Hapo awali
tulikuwa na Vituo vya Afya 586 ambavyo vilivyokuwa
vinaweza kutoa huduma za Upasuaji ni 120 tu lakini hivi sasa tumeweza kukarabati vituo 205
ambavyo vyote vitatoa huduma ya upasuaji, vitakuwa na wodi ya mama na mtoto,
vichomea taka, chumba cha kuhiadhia maiti, maabara pamoja na Wataalamu wa Afya”
Alisema Jafo.
Hivyo kwa kiasi
kikubwa tumetembea kwenye matokeo ya Tafiti hii inayowasilishwa leo na tuna
uhakika kwenye Tafiti ijayo matokeo yatakuwa tofauti na yalivyo sasa
tunajivunia jitihada hizi na tunawapongeza Ofisi ya Taifa ya
Takwimu kwa matokeo haya.
Wakati huo huo Mhe.
Seleman Jafo amewaagiza Watafiti nchini kuwa waadilifu katika kutafuta na kutoa
Takwimu sahihi ili Serakali iweze kujitathmini na kuweka mikakati katika utoaji
wa huduma katika jamii na kuleta maendeleo.
Amesema kuwa Takwimu
zikiwa sahihi na kuandikwa kwa weledi husaidia katika kuleta maendeleo kwa
jamii kwa kupanga bajeti zenye uhalisia kulingana na takwimu zilizotolewa
ambazo zinaonyesha mapungufu yaliyopo na jinsi ya kutatua mapungufu hayo.
“Takwimu husaidia
kupanga mikakati mbalimbali ya kuleta
maendeleo katika Taifa hivyo ni vyema zikawa sahihi na zinazolinda maslahi
mapana ya taifa kwa kuzingatia sheria na taratibu za nchi.” Amesema Jafo
Halkadhalika Mhe. Jafo amesemaTakwimu hii imeipa
Wizara mwelekeo ya kujipima kulingana na kazi mbalimbali za Afya zinazoendelea
kufanyika katika maeneo yote Nchini.
Wakati huohuo Bi.
Ruth Minja Kaimu Meneja wa Takwimu za Mazingira kutoka Ofisi ya Takwimu ya
Taifa (NBS) amesema National Evaluation
Platform (NEP) ni Jukwaa ambalo
linakusanya na kuchambua takwimu za afya na Lishe kutoka vyanzo mbalimbali ili
kuwezesha Serikali kupata majibu ya kimkakati
ya ushahidi ya kitakwimukatika utekelezaji wa Sera na Programu zote
zinazohusu afya ya lishe ya Mama
Mjamzito na Mtoto.
Amesema NEP linajumuisha
mkusanyiko wa mbinu mbalimbali za kitakwimu ambazo zinawasaidia wafanya maamuzi
kuainisha maswali ya kipaombele na kuyafanyia tathmini.
Aidha amebainisha
kuwa Uchambuzi umekusanya taarifa muhimu
ambazo zinasaidia kutambua kuwa ni afua zipi za afya zinafanya vizuri na kubainisha mapungufu katika utendaji ili kuweka mbinu na kubuni njia ya kuboresha huduma ya mama na
motto katika Lishe.
Kikao cha kupokea
matokeo ya utafiti wa huduma za afya Nchini iliyowasilishwa na Jukwaa la kukusanya na kuchambua takwimu za
afya na Lishe ( National Evaluation Platform-NEP) na kusimamiawa na Ofisi ya Takwimu ya Taifa
NBS kimefanyika leo katika ukumbi wa
TAMISEMI mjini Dodoma.
OR-TAMISEMI Yaenda Sambamba na Tafiti NBS
Reviewed by KUSAGANEWS
on
March 01, 2018
Rating:
No comments:
Post a Comment