Waziri wa mambo ya ndani Mwigulu Nchemba amewataka madereva
bodaboda kote nchini kufanya kazi ya bodaboda kuwa ya heshma kutokana na kazi
hiyo kuleta maendeleo makubwa kwa nchi kwa kurahisisha utoaji wa huduma na na
upatikanaji wa ajira kwa vijana.
Mwigulu ametoa wito huo Leo wakati akizungumza na madereva
bodaboda Mkoani Arusha baada ya kusikiliza taarifa ya marejeho ya mkopo
wa pikipiki uliotolewa kwa madereva bodaboda wa kata 25 za wilaya ya Arusha.
Amesema kuwa bodaboda ni hatua kubwa ya mafanikio ya nchi
hivyo wanapaswa kujivunia na kufanya shughuli ya heshima na sio shughuli
inayofanywa na watu waliokosa kazi za kufanya.
Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mrisho Gambo ameeleza kuwa
walifikia utaratibu wa kutoa bodaboda miambili zenye thamani ya millioni
mianne baada ya kuona kuwa madereva bodaboda ni watu ambao hawawezi
kupata fursa za kukopa kwenye mabenki kutokana na kutokukidhi vigezo na
masharti.
Naye Mwenyekiti wa umoja wa madereva wa bodaboda Jiji la Arusha
(UBOJA) Bwana Maulid Makongoro ameeleza kuwa pikipiki hizo
ziligawanywa kwa uwiano sawa kwa kata zote 25 za Jiji la Arusha ambapo
kila kata walipata pikipiki 8 na hadi sasa wamefanya marejesho ya zaidi ya
millioni mia tatu.
MWIGULU AWATAKA MADEREVA WA BODABODA KUFANYA KAZI KWA HESHIMA
Reviewed by KUSAGANEWS
on
March 03, 2018
Rating:
No comments:
Post a Comment