Tume ya utumishi wa
walimu wa shule za Msingi na Sekondari za umma nchini imesema itaendelea
kuwachukulia hatua za kinidhamu walimu ambao watabainika kufanya mapenzi na
wanafunzi pamoja na utoro kazini.
Akizungumza na Walimu wakuu wa Shule
za Msingi na Sekondari zaidi ya 100 Wilaya ya Kyela mkoa wa Mbeya Mwenyekiti wa
Tume ya utumishi wa walimu Tanzania, Bi. Oliver Muhaiki amesema mojawapo ya
kazi kubwa ya tume hiyo ni kusimamia maadili na wajibu wa walimu wanapokuwa
wakitekeleza majukumu yao.
Amesema baadhi ya walimu nchini
wamekuwa wanashindwa kuzingatia maadili ya kazi yao ikiwa ni pamoja na kufanya
mapenzi na wanafunzi na utoro kazini vitendo ambavyo amesema havipaswi
kuvumiliwa na tume hiyo.
Kwa upande wake Mkurugenzi wa Tume
ya walimu Mektirisi Kapinga amesisitiza umuhimu wa walimu kufahamu Muundo wa
tume hiya inapokuwa inasimamia masuala yanayowahusu walimu.
Aidha imebainishwa kwamba uwepo wa
tume hiyo ambayo ni maalumu tu kwa walimu wa shule za msingi na sekondari za
umma, kunawapa matumaini walimu wa Wilaya ya Kyela mkoani Mbeya kutatuliwa changamoto
zao.
WALIMU WANAOJIHUSISHA KIMAPENZI NA WANAFUNZI KUSHUGHULIKIWA.
Reviewed by KUSAGANEWS
on
February 01, 2018
Rating:
No comments:
Post a Comment