Mahakama ya Hakimu
Mkazi Mbeya imewatia hatiani mbunge wa Mbeya Mjini, Joseph Mbilinyi maarufu
Sugu na Katibu wa Chadema Kanda ya Nyanda za Juu Kusini, Emmanuel Masonga na
kuwahukumu kifungo cha miezi mitano jela.
Hukumu hiyo imetolewa leo Februari 26,2018 na Hakimu Mkazi Mfawidhi wa mahakama
hiyo, Michael Mteite.
Sugu na Masonga
wamehukumiwa kwa kosa la kutumia lugha ya fedheha dhidi ya Rais John Magufuli.
Wawili hao wanadaiwa
kutenda kosa hilo kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika Desemba 30,2017 eneo la
Uwanja wa Shule ya Msingi Mwenge jijini Mbeya.
No comments:
Post a Comment