| Katibu Mkuu OR-TAMISEMI Mhandisi Mussa Iyombe akizungumza na wajumbe wa Kikao Kazi(hawapo pichani) kabla ya kumkaribisha mgeni rasmi kufungua Kikao hicho. |
| Katibu Mkuu OR-Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala bora Dkt.Laurean Ndumbaro akizungumza na wajumbe wa Kikao Kazi cha kujadili mpango wa Utekelezajo wa Miradi ya LGDG. |
| Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe.Selemani Jafo (Mbele aliyesimama) akizungumza na wajumbe wa Kikao kazi cha kujadili mpango wa utekelezaji wa miradi ya LDGD |
| Baadhi ya Wakurugenzi wa OR-TAMISEMI wakibadilishana mawazo wakati wa Kikao kazi cha kujadili utekelezaji wa Miradi ya LGDG. |
NTEGHENJWA HOSSEAH, OR-TAMISEMI.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na
Serikali za Mitaa Mhe. Selemani Jafo
amewataka viongozi wa Halmashauri zote Nchini kupitia mipango iliyopo (Review)
na kupanga Upya Kimakati miradi yote ya maendeleo inayotekelezwa kwa Fedha za mfuko
wa Maendeleo ya Serikali Mitaa (LGDG).
Waziri Jafo ameyasema hayo kwenye Kikao Kazi cha
kujadili Mpango wa Utekelezaji wa Miradi ya LGDG iliyoboreshwa kwa
mwaka wa Fedha 2017/2018 kilichohusisha baadhi ya Wah. Wabunge, Mameya, Wenyeviti
wa Halmashauri, Wakurugenzi wa Mamlaka za Serikali za Mitaa pamoja na Maafisa
Mipango kilichofanyika katika chuo cha Mipango kilichopo mjini Dodoma.
Waziri Jafo alisema kuwa Bajeti ya Mfuko wa Maendeleo
ya Serikali za Mitaa kwa mwaka huu wa Fedha
ni Bil.251 ambazo hugawanywa kwa halmashauri zote Nchini. Fedha hizi ni nyingi
sana na zinatosha kutekeleza miradi michache yenye Tija na itakayopunguza
changamoto kwa wananchi wetu lakini kinachofanyika ni kuwa halmashauri
hugawanya kiasi wanachopata kwenye miradi mingi ambapo sio rahisi kuona matokeo
kwakuwa miradi mingi haikamiliki.
“Katika Halmashauri nyingi badala ya kugawanya Fedha hizi za Ruzuku kwenye
miradi mingi kwa viwango kidogo kidogo ni vyema sasa tukajieleza kwenye miradi
michahe ambayo tutahakikisha inakamilika kwa mwaka wa Fedha husika na kuanza
kutoa huduma kwa jamii” Alisema Jafo.
“Kuna miradi viporo mingi sana katika Halmashauri zetu
ukiangalia Sekta ya Afya utakutana
Maboma mengi ambayo yangekamilika yangetumika kama Zahanati au Vituo vya Afya,
Elimu utashuhudia magofu ya kutosha ambayo yangekamilika yangetumika kama
vyumba vya madarasa hii yote ni kutokana na kupanga miradi mingi kwa wakati
mmoja sasa kwa mwaka huu na kupitia Kikao hiki mfanye mapitio Upya na mpange
miradi michache itakayokamilika kupitia bajeti kwa mwaka huu” Aliongeza Jafo.
Waziri Jafo alisisitiza kuwa Katika Bajeti ya LGDG
mwaka huu Bil.66 zimeelekezwa kwenye Sekta ya Afya nataka mkazisimaie
mkakamilishe Maboma yaliyotelekezwa kwa kipindi kirefu na yakamilke tayari kwa
kutoa huduma halkadhalika katika maeneo mengine yote ambayo Fedha hizi
zitatumika.
Waziri Jafo alimalizia kuwa kikao hiki sio Semina wala
eneo la mapumziko kwa viongozi wa halmashauri
bali ni Kikao kazi hivyo Kitumike
kama fursa adhimu na muhimu ya kufanya
Mapitio ya Mipango ya halmashauri
ambayo ikitekelezwa italeta matokeo Chanya na kuwapunguzia adha
wananchi wetu.
Akimkaribisha Mgeni Rasmi Katibu Mkuu Ofisi ya Rais –
TAMISEMI Mhandishi Musa Iyombe amesema
Kikao hiki ni Maalumu kwa Viongozi wote ambao wanahusika moja kwa moja na
kuwaletea wananchi maendeleo ili kwa pamoja tukubaliane, tushauriane na
tuelekezane namna bora ya kutekeleza miradi hiyo ambayo inaonekana eneo la
Mipango halijafanyiwa kazi kikamilifu.
“Viongozi wenzangu lazima suala la mipango liangaliwe
kwa Makini katika Halmashauri zetu,
Jambo hili lisipofanyika kwa Umakini lina madhara makubwa kwa Jamii,
litaturudisha nyuma kimaendeleo na kila siku tutaona hatufanikiwa katika miradi
yetu kwa sababu tu tulikosa umakini katika kuandaa Mipango yetu, hebu tupitie
upya mipango yetu na tuhakikishe tunamaliza mradi mmoja kwanza kabla ya kuanza
mwingine” alisema Mhandisi Iyombe.
Akizungumza na wajumbe wa Kikao kazi Katibu Mkuu Ofisi
ya Rais-Menejiment ya Utumishi wa umma
na Utawala bora Dkt.Laurean Ndumbaro
amewakumbusha watumishi wote kufanya kazi kwa kuzingatia Hotuba ya Mhe.Rais Dkt. John Joseph Pombe Magufuli alipohutubia Bunge na
kusisitiza Uwajibikaji, Utumishi wa Umma unaojali misingi ya Uadilifu, Weledi
wa Kitaaluma, Maadili na Uadilifu katika Utendaji kazi wetu.
“Watumishi wanapaswa kuwajibika kwa Serikali iliyopo
Madarakani kwa kutekeleza yale yote yanayowapasa kutekeleza kwa mujibu wa
miongozo kwa watumishi wenzetu tunaofanya nao kazi na kwa wananchi
tunaowatumikia, tuwape haki yao ya msingi ya kuwahudumia na kuwalete maendeleo.”
Alisema Dkt. Ndumbaro.
Kupitia Kikao hiki washiriki kutoka katika Halmashauri
zote watapitia Upya miradi ya maendeleo waliyopanga kutekeleza kupitia Fedha za
“LGDG” kwa kuzingatia maelekezo
watakayopewa kabla ya kupokea Fedha hizo kwa ajili ya utekelezaji.
Miradi ya Maendeleo kufanyiwa mapitio ya Kimkakati
Reviewed by KUSAGANEWS
on
February 27, 2018
Rating:

No comments:
Post a Comment