Kesi za wabunge zatajwa tena

Kesi ya jinai inayowakabili wabunge wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo, Suzan Kiwanga (Mlimba), Peter Lijualikali (Kilombero) na watuhumiwa wengine 54 imepangwa kuanza kusikilizwa kwa mara ya kwanza Machi 28 katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Morogoro

Kesi hiyo ya jinai namba 296 ya Mwaka 2017 inaendeshwa na Hakimu Mkazi Ivan Msacky, ambapo washtakiwa wote 56 wanakabiliwa na mashtaka nane kila mmoja likiwemo la kufanya fujo kwenye uchaguzi mdogo wa udiwani Kata ya Sofi wilayani Malinyi na kusababisha uharibifu wa mali ikiwemo kuchoma moto ofisi za serikali ya Kijiji.

Hakimu Msacky amesema, upelelezi wa kesi hiyo umekamilika na pande zote mbili zimekubaliana kuanza kusikilizwa kwa kesi hiyo ifikapo Machi 28 mwaka huu,

Katika kesi hiyo upande wa Jamhuri unawakilishwa na Wakili Sunday Hyera akishirikiana na Edgar Bantulaki, ambapo upande wa utetezi unaongozwa na Barthlomew Tarimo, akishirikiana na Wakili Peter Kibatala.
Kesi za wabunge zatajwa tena Kesi za wabunge zatajwa tena Reviewed by KUSAGANEWS on February 27, 2018 Rating: 5

No comments: