Jeshi la Polisi Mkoa wa Morogoro
linawashikiliwa watuhumiwa zaidi ya 10 wa mauaji ya aliyekuwa diwani wa
Chadema, Kata ya Namwawala Wilaya ya Kilombero, Godfrey Lwena.
Akizungumza Kamanda wa Polisi mkoani hapa,
Ulrich Matei amesema watuhumiwa hao wanashikiliwa kwa uchunguzi na upelelezi
ukikamilika watafikishwa mahakamani.
Lwena aliuawa na watu wasiojulikana kwa
kukatwa na mapanga sehemu mbalimbali za mwili wake akiwa nyumbani kwake
Februari 22, 2018.
Matei amesema kwa sasa majina ya watuhumiwa
hayo yanahifadhiwa ili kutoharibu uchunguzi, na kwamba yatawekwa wazi baada ya
upepelezi kukamilika.
Awali, katika taarifa yake kwa nyombo vya habari kamanda Matei amesema mauaji hayo yanatokana na kisasi kufuatia kifo cha mkazi wa kata hiyo, Kennan Haule aliyeuawa na watu wasiojulikana mwanzoni mwa mwaka 2016
Amesema mtu huyo ameuawa kufuatia mgogoro wa
shamba uliopo kati ya wananchi na Bodi ya Sukari ambapo Lwena alinukuliwa
akiwaambia wananchi kuwa Haule asipokufa hawatapata haki yao na baada ya siku
kadhaa aliuawa.
Amebainisha kuwa eneo hilo lina migogoro ya muda
mrefu ya mashamba na watu wengi wameuawa katika mazingira yanayofanana
“Tunaendelea na uchunguzi wa kina
katika eneo lile la Namwawala na kata za jirani ili kubaini hao wanaoendesha
haya mauaji na wote watachukuliwa hatua za kisheria,” amesema Matei.
10 washikiliwa kwa mauaji ya diwani Chadema
Reviewed by KUSAGANEWS
on
February 27, 2018
Rating:
Reviewed by KUSAGANEWS
on
February 27, 2018
Rating:


No comments:
Post a Comment