Zaidi ya raia 800 kutoka jamhuri ya kidemikrasi ya Kongo wamewasili
mjini kigoma kuomba hifadhi ya ukimbizi nchini wakidai kukimbia
vita katika nchi hiyo.
Raia hao wa DRC ambao wengi ni wanawake na watoto wametokea
mashariki ya nchi hiyo na wamewasili kwa maboti kwa nyakati tofauti
katika bandari ndogo ya Kibirizi mjini kigoma na kueleza kuwa hali ya
vita katika nchi hiyo ni mbaya na kuomba serikali ya Tanzania
kuwapokea.
Mkuu wa mkoa wa Kigoma Brigedia Jenerali Mstaafu Emmanuel
Maganga akiambatana na kamati ya ulinzi na usalama ya mkoa
amefika katika eneo hilo na kueleza kuwa wamewapokea lakini
serikali inafanya tathmini ya ujio wao.
Zaidi ya raia 800 kutoka DRC Kongo wawasili kigoma kuomba hifadhi.
Reviewed by KUSAGANEWS
on
January 27, 2018
Rating:
No comments:
Post a Comment