Waziri Lukuvi atoa siku 7 kwa wakulima wa mbogamboga walioko ndani ya hifadhi ya uwanja wa ndege Mwanza

Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya makazi Mh.William
Lukuvi ametoa siku 7 kwa wakulima tisa wa mbogamboga walioko ndani ya hifadhi
ya uwanja wa ndege wa Mwanza kuondoka mara moja, huku akiwataka wananchi
wanaodaiwa kuvamia na kujenga makazi katika eneo la hifadhi ya uwanja huo kuwa
tayari kuondoka bila kusubiri fidia.


Waziri Lukuvi ametoa agizo hilo baada ya kutembelea maeneo yenye migogoro ya mpaka baina ya taasisi za serikali na wananchi katika halmashauri ya manispaa ya Ilemela mkoani Mwanza.

Halikadhalika, Mh. Lukuvi akizungumza na watumishi na wakuu wa idara za halmashauri ya manispaa ya Ilemela na jiji la Mwanza, wakati wa ziara ya kukagua mifumo ya ulipaji kodi ya ardhi na maendeleo ya zoezi la urasimishaji wa makazi ya viwanja vilivyopimwa, amezitaka halmashauri zote nchini kukamilisha zoezi la ukusanyaji wa kodi ya ardhi kabla ya aprili 30 mwaka huu.

Nje ya ukumbi wa manispaa ya ilemela, waziri lukuvi akajikuta anazongwa na baadhi ya wananchi wenye kero za migogoro ya ardhi.


Waziri Lukuvi atoa siku 7 kwa wakulima wa mbogamboga walioko ndani ya hifadhi ya uwanja wa ndege Mwanza Waziri Lukuvi atoa siku 7 kwa wakulima wa mbogamboga walioko ndani ya hifadhi ya uwanja wa ndege Mwanza   Reviewed by KUSAGANEWS on January 27, 2018 Rating: 5

No comments: