Wananchi katika jiji la Arusha wamekaribishwa kushiriki
kwenye maadhimisho ya wiki ya sheria nchini ambayo yanaanza kesho Januari 28 mpaka januari tarehe 31 mwaka huu.
Naibu Msajili wa Mahakama Kuu Arusha Anjel-Rumisha amesema Uzinduzi wa wiki
ya sheria unafanyika kesho kwa matembezi
yatakayojumuisha watumishi wa Mahakama na wadau wote wa sheria pamoja na
viongozi wa sekta mbalimbali; ambapo mgeni rasmi anatarajiwa kuwa mkuu wa mkoa
wa Arusha Mrisho Gambo.
Amesema matembezi hayo yataanzia katika viwanja vya
mahakama kuu Arusha hadi mahakama ya Mwanzo Arusha Mjini maarufu Maromboso;
hivyo amewaomba wananchi kushiriki katika maandamano hayo ambayo yanatarajia
kuanza saa moja na nusu asubuhi.
Rumisha ameongeza kuwa baada ya hapo watakuwa na wiki
nzima ya kutoa elimu na kusikiliza wananchi; ambapo kutakuwa na banda katika
mahakama ya mwanzo Arusha mjini ambapo hapo watakuwepo wataalamu mbalimbali wa
masuala ya kisheria.
WIKI YA SHERIA KUANZA KESHO JANUARI 28.
Reviewed by KUSAGANEWS
on
January 27, 2018
Rating:
No comments:
Post a Comment