Waziri wa Madini Angellah
Kairuki amesaini Kanuni za Sheria Mpya ya Madini ambapo Wakala wa
Jiolojia Nchini (GST) amepewa nguvu ya kisheria ya kuingia katika ardhi yoyote
kufanya utafiti wa kina wa madini.
Akizungumza Naibu Waziri wa Madini Dotto Biteko amesema
kuwa kanuni hizo zimesainiwa Januari 9 mwaka huu ikiwa ni siku moja baada
ya Rais John Magufuli kuagiza kukamilishwa kwa mchakato wa kanuni hizo ndani ya
siku tano
Biteko alikuwa akizungumza mbele ya
Kamati ya Bunge ya Nishati na Madini ambayo ilitembelea ofisi za GST mjini
Dodoma.
Kuna watu wanasema sheria hii mpya
itafukuza wawekezaji na hakuna wawekezaji wapya watakaokuja lakini nataka
kuwaambia kuwa kuna wageni wengi wanakuja kutaka kuwekeza katika migodi
mikubwa,” amesema.
Amesema wastani katika kila
wiki wamekuwa wakipokea wawekezaji kati ya 10 na 20 ambao wanaonyesha nia ya
kuwekeza nchini katika sekta hiyo kwa hiyo sheria sio kikwazo kwao.
Alisema kujitokeza kwa wingi kwa
wawekezaji kunatokana na sheria hiyo kuweka uwazi katika taratibu na
kanuni za kuwekeza.
Biteko amesema lengo la wizara
yake ni kuongeza uchangiaji wa sekta ya madini katika pato la taifa kutoka
asilimia 4.8 ya mwaka jana hadi kufikia asilimia 10 kama Mpango wa Maendeleo wa
miaka mitano unavyosema.
Mbunge wa Tarime vijijini (Chadema)
John Heche amesema kampuni kubwa zinazokuja nchini kwa ajili ya uwekezaji
katika sekta hiyo, yanafanya utafiti kwa kipindi kirefu sana huku Serikali
ikiwa hainufaiki.
Wengine wanakuja kufanya utafiti kwa
zaidi ya miaka 10 na bado wakiondoka wanasema hawajapata kitu. Sisi tuna watu
wetu hapa (GST) wapewe mamlaka ya kisheria ya kufanya Exploration (utafiti wa
kina) na wawekezaji wanapokuja wapewe leseni za uchimbaji,” amesema.
Kauli hiyo iliungwa mkono na Makamu Mwenyekiti
wa Kamati hiyo, Deo Ngalawa (Ludewa-CCM) ambaye amesema kuwapa GST jukumu la
kufanya utafiti wa kina kutaongeza mapato kwa sababu wawekezaji watakapokuja
kuwekeza watalipia gharama za utafiti
Waziri Kairuki asaini kanuni mpya ya madini
Reviewed by KUSAGANEWS
on
January 28, 2018
Rating:
No comments:
Post a Comment