Watu 4 wafariki Dunia kwa Kufukiea na Kifusi cha Mchanga

Watu wanne wamefariki dunia na moja kujeruhiwa baada ya kuangukiwa na kifusi cha mchanga aina ya Moramu katika machimbo ya mchanga yaliyopo kata ya Murieti jijini Arusha wakati wakipakia mchanga katika machimbo hayo.

Tukio hilo limetokea mapema leo,jan,30 majira ya saa tano asubuhi katika eneo la mlima wa ccm Kata ya murieti

Marehemu  wametambulika kwa majina ya  Yusufu Mohamed Kamwende(35),Athumani Husein Luvanda,na Richard Kishimbo(57) na mmoja bado hajatambulika

Katika tukio hilo dereva wa gari lililokuwa likipakia Moramu aliye tambulika kwa jina moja la Hamisi alipata majeraha sehemu za kichani na kuvunjiaka mkoano ambapo amelazwa katika hospitali ya mkoa Mount Meru kwa matibabu zaidi.

Mashuhuda wa tukio hilo akiwemo diwani wa kata ya Muriet,Francis Mbise ameeleza kuwa marehemu walifariki dunia wakati wakipakia Moramu katika gari hilo ndipo ghafla ngema ilipokatika na kuwafunika ,

Aidha aliongeza kuwa gari aina ya Isuzu mali ya majeruhi iliyokuwa ikipakia Moramu hiyo iliharibika vibaya  .

Kamanda wa polisi Mkoa wa Arusha Charles Mkumbo amethibisha tukio hilo na kusema kwamba si mara ya kwanza kutukea tukio kama hilo ambapo amewataka wataalamu kutoka jiji la Arusha kutembelea katika machimbo hayo na kutoa tathimini iwapo machimbo hayo yanafaa kuendelea kuchimbwa ama yasitishwe ili kuepuka maafa zaidi kama hayo yanayoweza kujitokeza.

Aidha amewataka wajimbaji wa Moramu kuchukua tahadhali pale wanapoona kuna tishio  la ngema kumeguka ili kuepuka na hatari iliyopo mbele yao
.
Watu 4 wafariki Dunia kwa Kufukiea na Kifusi cha Mchanga Watu  4 wafariki Dunia kwa Kufukiea na Kifusi cha Mchanga Reviewed by KUSAGANEWS on January 30, 2018 Rating: 5

No comments: