UWT WAADHIMISHA MIAKA 41 YA CHAMA CHA MAPINDUZI KWA KULA NA WATOTO YATIMA NA KUFANYA USAFI SOKONI



Mjumbe wa baraza kuu la jumuiya ya Wanawake UWT Taifa Bi Ana Msuya akiwa amebeba mtoto yatima walipokwenda kuwatembelea katika kituo cha Genesis Kilichopo Kisongo kata ya mateves
picha ya pamoja ya wanawake wa UWT waliotembea kituo cha kelelea watoto yatima
Watoto yatima wanaolelewa katika kito cha genesisi Kisongo kata ya mateves


Na Alphonce Saul

Umoja wa wanawake wa UWT wilayani Arumeru mkoani Arusha wamejitokeza kufanya usafi kwenye Soko la Kisongo Pamoja na kutembelea kituo cha watoto yatima cha GENESIS na kushiriki nao chakula cha Mchana katika kata ya  Mateves kwa lengo la Kuadhimisha miaka 41 ya chama cha Mpinduzi.

Akizungumza Mjumbe wa baraza kuu la jumuiya ya Wanawake UWT  Taifa Bi Ana Msuya amesema kuwa wameona wasiadhimishe peke yao bali kwa kushiriki kwa kufanya shughuli za kijamii ambazo zinawagusa moja kwa moja.

Bi Ana amesema kuwa changamoto zilizopo katika kituo hicho cha watoto Yatima ni ukosefu wa maji lakini yeye kama kiongozi atahakikisha anafuatilia suala hilo kwa kuzungumza na mamlaka husika ili kupeleka huduma ya maji kwenye kata hiyo ya Mateves.

Hata hivyo ameongeza kuwa kama jumuiya ya wanawake UWT wa chama cha mapinduzi CCM kazi yao ni kuona wanafikia watu wanaoshi kwenye mazingira magumu na wenye uhitaji ili kuwasaidia pale wanapoguswa.

Kwa upande wa mjumbe wa halmashauri kuu wilaya ya Arumeru Bi Tausi Swalehe amesema kuwa kutoa ni tabia lakini pia si lazima uwe na fedha nyingi ndipo utoe bali ni kuwa na utaratibu na moyo wa kusaidia kwa karibu makundi maalum wakiwemo yatima.

Naye Mary ambaye ni mlezi wa watot yatima katika kituo hicho cha Genesis amepongeza umoja huo wa UWT na amesema kuwa mpaka sasa katika kituo hicho wana wanalea watoto 28 ambao mmoja kati yao ana miezi wamiezi mitatu ambaye alitelekezwa na mama yake mzazi eneo la Ngaramtoni.

Hata hivyo amesema kuwa changamoto kubwa wanayokutana nayo ni ukosefu wa huduma ya maji ambapo wanateseka kutokana na uhitaji wao pamoja na huduma za afya na kuomba serikali iangalie pia vituo hivyo vya kulelea watoto Yatima.




UWT WAADHIMISHA MIAKA 41 YA CHAMA CHA MAPINDUZI KWA KULA NA WATOTO YATIMA NA KUFANYA USAFI SOKONI UWT WAADHIMISHA MIAKA 41 YA CHAMA CHA MAPINDUZI KWA KULA NA WATOTO YATIMA NA KUFANYA USAFI SOKONI Reviewed by KUSAGANEWS on January 30, 2018 Rating: 5

No comments: