Wanachama wa chama cha Ushirika cha Uru Kati
Mawela, wamemuomba Rais John Magufuli, kuingilia kati mgogoro wa ardhi
wakihofia kufilisiwa shamba walilopewa na Serikali lenye ukubwa wa hekari
213.
Wasiwasi huo unatokana na
kushindwa kesi waliyoifungua dhidi ya kampuni ya mwekezaji, Laitolya Tours
& Safaris, ambayo imejenga hoteli ya kitalii ya Kilemakyaro Mountan
Lodge ndani ya hekari 27.54.
Hayo yamejitokeza katika mkutano
mkuu maalum wa wanachama ulioitishwa leo Januari 27, mahsusi kujadili hukumu
hiyo iliyotolewa Ijumaa ya Januari 19 na Jaji Benedict Mingwa wa Mahakama Kuu
Moshi.
Katika hukumu hiyo, Jaji Mingwa
amesema hekari hizo 27.45 ni mali ya Laitolya Tours and Safaris na
kuutaka ushirika huo kukabidhi hati namba CT10663 ili kampuni imilikishwa
hekari hizo 27.54.
Mbali na kuamuru hati hiyo
ikabidhiwe kwa msajili wa hati, lakini Jaji Mingwa ameamuru pia kuwa wana
ushirika hao watalazimika kulipa gharama za kesi hiyo ya madai namba 10 ya
mwaka 2015.
Hata hivyo, Mrajisi Msaidizi wa
vyama vya Ushirika mkoa Kilimanjaro, Henjewele John, ameliwaambia wanachama
hao kuwa mwekezaji huyo amempibu Rais Magufuli na kwamba atampigia simu.
Niwaahidi kwamba tutatumia njia
zote kuhakikisha kuwa wananchi wa Uru wanapata haki yao. Hapa tutamwambia
Ushirika leteni hati yenu ya kumiliki na huyu mwekezaji alete hati
zake,”amesema.
Sasa hivi nataka niwaambie majumba
ya watu yanabomolewa. Si mnaona? Kwa hiyo huyu mzee wetu amebipi sasa akibipu
sisi tutapiga. Zama zimebadilika na kwa hili tutalifikisha kwa
Rais,”amesisitiza.
Mwenyekiti wa Ushirika huo,
Richard Kimaro, amesema wao hawakuwahi kumpa mwekezaji huyo eneo hilo la
ardhi, bali walimkodishia lakini aliwazunguka kwa kushirikiana na baadhi ya
viongozi.
“Katika kipindi chote cha mkataba
tangu 1998 hakuwahi kulipa kodi ya pango ambayo kwa mujibu wa mkataba ilikuwa
Dola 700 za Marekani (sawa na Sh1.6 milioni) kwa mwezi,”alidai mwenyekiti
huyo.
Kwa mujibu wa mwenyekiti huyo, ni
kutokana na kutolipa kodi hiyo na kujimilikisha ardhi yao, walifungua kesi ya
madai wakitaka ushirika ulipwe malimbikizo ya kodi yanayofikia Dola 153,600.
Mbali na kudai fedha hizo, lakini
waliiomba mahakama itamke kuwa mwekezaji huyo ni mvamizi na ameingia kwa
jinai katika shamba lao na pia imuamuru alipe fidia ya jumla ya Sh80 milioni.
Akizungumza katika mkutano huo,
mmoja wa wanachama wa Ushirika huo, Francis Moshi, alisema wamekanganyikiwa
waliposikia wameshindwa kesi na kudaiwa kuwa wao ndio walivuruga mkataba
Tunajiuliza hivi ni nani hapa alivuruga
mkataba kati yetu na Laitolya ambaye hakulipa kodi ya pango kwa mujibu wa
mkataba? Ulikuwa mkataba wa miaka 10 akaongeza sifuri ukawa miaka
100,”amedai.
Makamu Mwenyekiti wa Ushirika huo,
Emanuel Mushi, alisema kilichojificha ni kuwa baadhi ya viongozi walishiriki
kughushi muhtasari wa vikao mbalimbali kwa maslahi ya mwekezaji huyo.
Wajumbe wa mkutano huo waliazimia
kwa kauli moja, kwamba bodi ya uongozi ya chama hicho ikate rufaa kupinga
hukumu hiyo na pia ilipeleke suala hilo ngazi za juu Serikalini kupitia kwa
Mrajisi.
Hata hivyo mkurugenzi wa kampuni
hiyo, Joachim Minde alipotafutwa jana, alisema anawashangaa wanachama hao
kufanya mkutano badala ya kukata rufaa kama hawakuridhika na uamuzi.
Wao kama wanataka kwenda kwa Rais
sijui Waziri wa Ardhi wao waende. Kama mimi nina haki yangu si lazima
nitalalamika? Wao kama nao wanaona wana haki walalamikie mahakama,”amesema.
“Huwezi kulalamika kuwa unamtaka
Rais sijui unamtaka Waziri. Hili jambo sio la leo. Alishakuja Waziri wa
Ushirika na pia akaja Waziri wa Ardhi hapa. Sio jambo geni
kabisa,”amesisitiza Minde.
Minde amedai kuwa kinajitokeza ni
kwamba wamekuja baadhi ya viongozi wa Ushirika ambao ni wageni wanaosumbuliwa
na njaa na atafurahi sana kama siri ya mgogoro mzima ujulikane
Mkurugenzi huyo alisema huu ni
wakati wa kujua mapato na matumizi ya shamba hilo na kwamba kwa sasa
anajiandaa kufungua kesi nyingine ya madai kwa jinsi walivyopata hasara tangu
1998
|
Wanachama wampigia magoti Raisi
Reviewed by KUSAGANEWS
on
January 27, 2018
Rating:
No comments:
Post a Comment