Baada ya waziri mwenye dhamana ya mifugo na uvuvi juzi
kukamata tani 7 zenye thamani ya shilingi milioni 100 kwenye kiwanda cha
Sunflag kilichopo njiro mkoani Arusha leo tena wizara hiyo imekamata tani zaidi
ya 50 zenye thamani ya zaidi ya shilingi milioni 300 katika kiwanda hicho.
Akizungumza afisa wa doria katika wizara ya mifugo na
uvuvi Bwana West Mbembati amesema kuwa tarehe 17 na 18 walifika kwenye kiwanda
hicho na kubaini tani 7 za nyavu haramu
na kiwanda hicho kikapigwa faini lakini walikuwa wameficha nyingine stoo.
Mbembeti amesema kuwa kiwanda hicho kimekwenda kinyume
na sheria namba 22 ya mwaka 2003 na kanuni za uvuvi za mwaka 2009 kifungu namba
80.
Hata hivyo ameongeza kuwa wafanyakazi wanaofanya kazi
kwenye kiwanda hicho wamekosa uzalendo kwa kuwa wao ndo walikuwa wanazalisha
lakini hawatoi taarifa kuhusu nyavu hizo haramu jambo ambalo linasikitisha.
Amesema kuwa tayari wanamsubiri waziri mwenye dhamana ya
nifugo na uvuvi Mh Luhaga Mpina kufanya maamuzi baada ya kubaini nyavu hizo.
TANI ZAIDI YA 50 ZA NYAVU HARAMU ZAKAMATWA KWENYE KIWANDA CHA SUNFLAG ARUSHA NJIRO
Reviewed by KUSAGANEWS
on
January 22, 2018
Rating:
No comments:
Post a Comment