Katibu wa
Itikadi na Uenezi wa CCM, Humphrey Polepole amewataka viongozi wa chama hicho
Manispaa ya Moshi, kuacha kutembea na watu mifukoni na kutengeneza kofia za
ubaguzi ndani ya chama kwa kuwa hali hiyo imekuwa ikikigharimu chama wakati wa
uchaguzi.
Polepole
amesema chama hicho kimekuwa kikijikuta katika wakati mgumu wakati wa uchaguzi
kutokana na baadhi ya viongozi ndani ya chama kupenda ubinafsi na kuweka mbele
uheshimiwa badala ya utumishi.
Ametoa
rai hiyo leo Jumamosi wakati akizungumza kwenye kikao cha ndani cha
Halmashauri Kuu ya CCM Manispaa ya Moshi kilichofanyika mjini Moshi katika
ukumbi ulioko kwenye ofisi za chama hicho mkoa ambapo amesema sasa ni wakati wa
kujiimarisha ili kuweza kushika hatamu kila ngazi.
Amesema
kumekuwepo na baadhi ya viongozi ndani ya chama ambao wamekuwa wakitengeneza
makundi ya walionacho na wasio nacho wakati wa uchaguzi hali ambayo imekuwa
ikikifanya chama kushindwa kila mwaka wa uchaguzi katika majimbo
mbalimbali likiwemo jimbo la Moshi Mjini.
Kushindwa kwa
CCM katika majimbo mengi Kilimanjaro hasa hili la Moshi Mjini,
kulisababishwa na viongozi, kutembea na majina yao mifukoni na kuweka
uheshimiwa mbele badala ya utumishi, hali hii ilijenga makundi, sasa ni
lazima tubadilike," amesema Polepole
POLEPOLE VIONGOZI WENGI WANAPENDA UHESHIMIWA BADALA YA UTUMISHI
Reviewed by KUSAGANEWS
on
January 20, 2018
Rating:
No comments:
Post a Comment