MSHUKIWA wa ulaghai
Alhamisi aliomba korti imwachilie kwa dhamana ndogo kwa vile anaugua ugonjwa wa
Saratani.
Bi Lilian Awuor alimsihi
hakimu mwandamizi Bi Martha Mutuku amwonee huruma na kumwachilia kwa dhamana
isiyo ya juu akitilia maanani ni “mgonjwa sana”.
“Ikiwa nitapewa dhamana
ya kiwango cha juu, sitaweza kuipata kwa vile naugua maradhi ya Saratani na
yamenigharimu pesa nyingi,” Bi Awuor alimweleza hakimu.
“Je una hati yoyote
kuonyesha unaendelea kupokea matibabu ya Saratani?” Bi Mutuku alimwuliza.
“Ndio niko na
ushahidi," alijibu Awuor; kisha akampa stakabadhi kutoka hospitali
anakoendelea kupata matibabu,
Mshtakiwa aliyekanusha
shtaka la kupokea kwa njia ya undanganyifu vipande 25,000 vya sabuni ya Jamaa
vyenye thamani ya zaidi ya Sh3.3 milioni pamoja na kupokea pesa tasilimu
Sh105,000 kutoka kwa mlalamishi Bi Emily Awino aliachiliwa kwa dhamana ya pesa
taslimu Sh50,000.
Kesi itasikizwa Februari
23, 2018.
MSHUKIWA WA ULAGHAI WA SABUNI YA SH3.3 MILIONI AACHILIWA KWA DHAMANA YA SH50,000 PESA TASLIMU
Reviewed by KUSAGANEWS
on
January 25, 2018
Rating:
No comments:
Post a Comment