WAZIRI wa Usalama wa Ndani Dkt Fred Matiang’i Alhamisi alikana vikali madai kuwa ana uhusiano wa kimapenzi na msichana wa kanisa.
Kupitia msemaji wa Wizara ya Usalama wa Ndani Mwenda Njoka, Dkt Matiang’i alitishia kuishtaki kampuni ya Standard Group iwapo haitamuomba radhi kwa kuchapisha uvumi huo.
Bw Njoka alisema maelezo ya habari husika yalitumia sifa ambazo zinaweza kumfanya mtu yeyote mwenye akili timamu kujua ni Dkt Matiang’i anayezunguziwa.
“Japo gazeti lenu halikutaja jina la waziri husika, maelezo na maeneo yaliyochapishwa, yametumiwa awali na gazeti hilo kumwelezea Waziri Fred Matiang’i. Hii inaweka wazi kuwa waziri aliyetajwa si mwingine ila ni Dkt Fred Mataing’i,” Bw Njoka alisema katika taarifa yake.
Waziri huyo alisema habari iliyochapishwa ililenga kumharibia jina na kutaka gazeti hilo limuombe msamaha.
“Madhumuni ya barua hii ni kutaka habari hizo ziondolewe na msamaha kuchapishwa kwa muda wa siku saba,” taarifa hiyo ilinukuu

MATIANG'I AKANA KUWA NA UHUSIANO WA KIMAPENZI NA MSICHANA WA KANISA
Reviewed by KUSAGANEWS
on
January 25, 2018
Rating:
No comments:
Post a Comment