Kesi inayomkabili Mbunge wa Singida
Mashariki (Chadema), Tundu Lissu na wahariri wa Gazeti la Mawio katika Mahakama
ya Hakimu Mkazi Kisutu, imeahirishwa hadi Februari 26.
Wakili wa Serikali, Elia Athanas
jana alimueleza Hakimu Mkazi Mkuu, Thomas Simba kuwa kesi imepangwa kwa ajili
ya kutajwa na kwamba hadi sasa hawajajua hali ya mshtakiwa wa nne, Lissu.
Kesi hiyo ambayo ipo katika hatua ya
usikilizwaji wa ushahidi wa upande wa mashtaka, inamkabili Lissu na wenzake
Simon Mkina, Jabir Idrisa na Mchapishaji wa Kampuni ya Jamana, Ismail Mehbooh
Kwa pamoja washtakiwa hao,
wanakabiliwa na mashtaka matano likiwamo la kuandika habari za uchochezi
kinyume na Sheria ya Magazeti ya Mwaka 2002.
Inadaiwa kuwa Januari 12 hadi 14,
2016 jijini Dar es Salaam, washtakiwa Jabir, Mkina na Lissu, waliandika na
kuchapisha taarifaza uchochezi zenye kichwa cha habari kisemacho, ‘Machafuko
yaja Zanzibar.’
Katika shtaka la pili wanadaiwa kuwa
Januari 14, 2016 walichapisha habari hizo ili kuleta chuki kwa wananchi wa
Zanzibar.
Mshtakiwa Mehboob anadaiwa kuwa
Januari 13 ,2016 katika jengo la Jamana lililopo Manispaa ya Ilala, alichapisha
gazeti la Mawio lililokuwa na taarifa za uchochezi.
Kesi ya Lissu kuendelea Februari
Reviewed by KUSAGANEWS
on
January 25, 2018
Rating:
No comments:
Post a Comment