Baraza la madiwani wa halmashauri ya Arusha wamehoji kuhusu madiwani wanaojiuzulu nafasi zao na kuajiriwa katika kata mbalimbali kama watendaji wa kata.
Akihoji katika kikao cha robo ya NNE kwa mwaka wa Fedha 2016 / 2017 Diwani wa kata ya Olturoto Bwana Baraka Simon katika maswali na majibu amehoji ni kwanini madiwani wanaojizulu wanajiriwa kwenye kata kama siyo Rushwa.
Akijibu swali hilo Mkurugenzi WA halmashauri ya Arusha Dokta Wilson Mahera amesema kuwa taarifa hiyo ya kuajiriwa madiwani si za kweli Bali wameomba kujitolea kwenye baadhi ya kata za halmashauri ya Arusha.
Naye Mwenyekiti wa halmashauri hiyo bwana Noah Lembris amesema kuwa suala hilo linatazamwa kama rushwa kwasababu haiwezekani MTU ajiuzulu na apewe nafasi japo Mkurugenzi anasema ni kujitolea.
""Haiwezekani MTU anajiuzulu na kupewa nafasi ya kujitolea hapo inaonekana kuna harufu ya rushwa naomba Mkurugenz jambo hilo lifuatiliwe vizuri ili kujua ukweli wake""

No comments:
Post a Comment