Mahakama
ya juu ya kikatiba nchini Korea Kusini imemng’oa madarakani rais wa
nchi hiyo Park Geun-hye kwa tuhuma za rushwa. Mahakama hiyo imechukua
uamuzi huo baada ya majaji wake wengi kupiga kura za kuunga mkono
maamuzi ya bunge la Korea Kusini ya kumng’oa Park, ambaye ni mwanamke wa
kwanza kuliongoza taifa hilo.
Park alihusishwa na kujipatia
fedha kwa njia za ufisadi kutoka katika makampuni makubwa nchini humo
akishirikiana na rafiki yake Choi Soon-Sil. Kufuatia tuhuma hizo, Park
huenda akakabiliwa na mashtaka ya uhalifu.
Park
mwenye umri wa miaka 64, anakuwa rais wa kwanza kuchaguliwa
kidemokrasia Korea Kusini na kuondolewa madarakani, na kuwa rais wa pili
kuondolewa madarakani kutokana na tuhuma ambapo mwaka 2004 Rais Roh
Moo-hyun aliondolewa madarakani na bunge la nchi hiyo lakini alirudishwa
na mahakama miezi miwili baadaye.
MAHAKAMA YAMNG’OA RAIS WA KOREA KUSINI
Reviewed by KUSAGANEWS
on
March 12, 2017
Rating:
No comments:
Post a Comment