Watangazaji
wa kipindi cha Clouds 360 cha Clouds TV wakiongozwa na Babbie Kabae na
Sam Sasali wamemkabidhi msanii na mtayarishaji wa muziki nchini Jetman
hundi ya shilingi milioni 15 kutokana na michango iliyotolewa na watu
mbalimbali kwaajili ya matibabu yake.
Michango hiyo imekusanywa kutokana na kampeni iliyoanzishwa na kituo hicho iliyopewa jina la Amka na Jetman.
Wakati
huo huo mbunge wa jimbo la Nyamagana, Stanslaus Mabula amechangia kiasi
cha shilingi milioni tano kwa ajili ya matibabu hayo. Kiasi cha
takribani milioni 20 kimekusanywa katika kampeni hiyo.
Jetman amekuwa kitandani kwa takriban miaka mitano kutokana na tatizo la kupooza mgongo.
CLOUDS 360 WAMEMKABIDHI JETMAN MILLIONI 15
Reviewed by KUSAGANEWS
on
March 12, 2017
Rating:
No comments:
Post a Comment