Mwenyekiti wa Taifa wa Bodi ya
Parole,Dkt. Augustine Mrema amemwandikia barua Waziri Mkuu wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania, Mh. Kasim Majaliwa kulalamikia jeshi la Magereza
kukwamisha mpango wake wa kuwatoa wafungwa ambao tayari wameshalipiwa fedha na
wasamalia wema baada ya kukidhi vigezo.
Dkt. Mrema ameyasema hayo mchana huu
wakati wa kutoa taarifa yake hiyo kwa waandishi wa Habari Jijini Dar es Salaam
kuzungumzia suala lake hilo la Maafisa wa Magereza kusitisha hatua ya kukatisha
mpango wake licha ya kuwalipia wafungwa waliokidhi vigezo.
“Mimi nimeona nisinyamaze. Napaza
sauti nataka Rais aone, ajue kama magereza yetu yanashida na tunalotatizo kwa
nini mpango huu umesimamishwa na umesitishwa tumekosea wapi?.
"Nimesha muandikia barua Waziri
Mkuu kulalamikia jeshi la Magereza kukwamisha mpango huu na watu 43 tayari
tumesha walipia faini hiyo lakini bado wapo magerezani wanasota. Mrema amefanya
kosa lipi? Ama Mama Mchungaji Getrude Rwakatare amekosa nini? Mpaka wamesitisha
zoezi hili” amesema Mrema kwa waandishi wa habari.
Dkt. Mrema ameweza kuonyesha nyaraka
ikiwemo risiti mbalimbali walizofanya malipo kwa ajili ya kuwatoa wafungwa hao
ambapo amesema haki ya kuzuia mpango huo imeweza kumuumiza vibaya kwani
wasamalia wema walioweza kujitolea fedha za mpango huo imewagusa pia.
Pia ameongeza kuwa, mpaka sasa
magereza mbalimbali kuna msongamano wa wafungwa ambao wanahitaji msaada wa
kutoka ila hawajapata fedha za kulipiwa hivyo pindi wasamalia wema kama
Mchungaji Mama Rwakatare wanapojitokeza wanatakiwa kupongeza na wala si kupinda
kona kona.Hivi karibuni Jeshi la Magereza lilisitisha shughuli iliyokuwa
ikiendeshwa na Mchungaji Getrude Lwakatare ya kuwalipia faini wafungwa walioko
magerezani hadi hapo utaratibu mwingine utakapotolewa.
Awali ilidaiwa kuwa Mpango huo
unaofanywa na Lwakatare kwa kushirikiana na Mwenyekiti wa Taifa wa Bodi ya
Parole, Augustine Mrema tayari umewezesha wafungwa 78 kutoka magerezani baada
ya kuwalipia faini inayofikia Sh25 milioni.
Kwa mujibu taarifa zilizonukuliwa
katika moja ya vyombo vya habari hapa nchini vilieleza kuwa, Mkuu wa Magereza
Mkoa wa Dodoma, Antonio Kilumbi alisema amepata maelekezo ya kusitishwa kwa
mpango huo kutoka ngazi ya juu ya jeshi hilo na kuongeza kuwa, wananchi
wengine bado wanaweza kuwalipia faini hiyo ndugu zao.
Hata hivyo Mrema alisema
mpango huo ulilenga kupunguza msongamano magerezani na kuipunguzia Serikali
gharama za kuwahudumia wafungwa hivyo kusitisha unarudisha nyuma juhudi za Bodi
hiyo ya Parole katika kuwasaidia wafungwa waliokizi vigezo
Mwenyekiti wa Parole Augustine Mrema kumshtaki Mkuu wa Magereza Dodoma kwa Waziri Mkuu
Reviewed by KUSAGANEWS
on
November 17, 2016
Rating:
No comments:
Post a Comment