MWANAFUNZI WA UTAMADUNI KATIKA CHUO CHA MAKUMIRA ARUSHA AUWAWA KINYAMA



MSANII wa Nyimbo mbalimbali za kiutamaduni anayefanya shughuli zake ndani ya Kituo cha Utamaduni kilichopo Chuo Kikuu cha Makumira Wilayani Arumeru Mkoani Arusha, Juliana Issa (22)amekutwa ameuwawa na watu wasiojulikana kisha mwili wake kutupwa kwenye majaruba ya mpunga.

Aidha  mwili huo wa Juliana ulikutwa mtupu na pembeni yake kulikuwa na nguo zake ambapo uchunguzi wa awali umebaini kuwa  mwili wake umekutwa na alama za kucha shingoni na uvimbe sehemu za siri.

Akizungumza na waandishi wa habari ofisi kwake jana Jijini Arusha, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha, Charles Mkumbo alisema tukio hilo lilitokea juzi saa 11:30 asubuhi eneo la Makumira.

Alisema taarifa za awali zinaeleza kuwa Novemba 1 mwaka huu muda wa saa 18:30jioni marehemu aliondoka nyumbani kwake kwenda kwenye Sherehe ya kuzaliwa "Birthday Party" ya rafiki yake ambayo ilipangwa kufanyika kwenye baa iitwayo V. I. C iliyopo eneo la Kilala lakini hakuonekana katika sherehe hiyo.

Siku ya pili Novemba 2,polisi walipata taarifa juu ya kuwepo kwa mwili ambao umekatwa kando kando ya barabara ya kuelekea Ndolo Lodgge, baada ya askari kufika eneo hilo walikuta mwili huo ukiwa mtupu na pembeni yake kulikuwa na nguo zake.

Alisema uchunguzi wa awali ulionyesha kuwa mwili huo ulikutwa na alama za kucha shingoni na uvimbe sehemu za siri kitendo kinachoashiria alikuwa amebakwa.

Alisema hadi sasa chanzo cha kifo hicho bado hakijajulikana na hakuna mtuhumiwa yoyote aliyekamatwa huku msako unaendelea ili kuwabaini wahusika wa tukio hilo huku mwili wake ukiwa umehifadhiwa hospitali ya Mount Meru kwaajili ya kufanyiwa uchunguzi wa daktari.
Awali mwandishi wa habari hii alifika kituo cha Utamaduni kilichopo Chuo kikuu cha Tumaini Makumira Wilayani Arumeru kwaajili ya kujua kama Juliana alikuwa ni mwanafunzi wa chuo hicho au la na nilizungumza na Mratibu wa Kituo hicho cha Sanaa(CAC), Randy Stubbs ambaye alisema amehuzunika na kifo cha msanii huyo ambaye yeye ni kama mwanae aliyemuasili.

Alisema juzi alimuomba ruhusa kuwa anakwenda kwenye sherehe ya kuzaliwa ya rafiki yake hakumtaja jina wala hakunitajia lakini hakurudi nyumbani kila nikimpigia simu haipokelewi na baadaye haiiti kabisa.

Alisema walihangaika pamoja na wasanii wenzake zaidi ya 25  wa kituo hicho kumtafuta bila mafanikio na juzi majira ya saa 11:30 asubuhi walipata taarifa kuwa mwili huo umepatikana maeneo hayo.

Alisema msiba huo ni pigo kwao na wanasubiri taarifa za polisi na hospitali ili waweze kufanya taratibu za mazishi ila nimeumia sana kama baba mlezi wa mtoto huyo pamoja na hawa wasanii wenzake kwakweli sijui ni nini.

Wakati huo huo, Mfanyakazi wa Ndani aitwaye Mary Simon (16),amejinyonga kwa kutumia mtandio wake hadi kufa baada ya kumpiga kichwani kofi mtoto Julius Thomas hawakusema umri wake na kuulizwa na Julius kwanini alimpiga kisha akamrudishia Mary kibao kichwani.

Mkumbo alisema baadaye Mary aliingia chumbani na kujifungia baada ya muda simu yake ya mkononi iliita hivyo mtoto wa mwenye nyumba aitwaye Enoth Frank alimpelekea lakini alikuta mlango umefungwa na akaamua kuzunguuka dirishani na kuchungulia ndipo alipomuona Mary akiwa amening'inia kwakutumia mtandio.

Mwili umehifadhiwa hospitali ya Mount Meru kwa uchunguzi zaidi huku chanzo cha kifo kikiwa bado hakijafahamika na upelelezi unaendelea. 
MWANAFUNZI WA UTAMADUNI KATIKA CHUO CHA MAKUMIRA ARUSHA AUWAWA KINYAMA MWANAFUNZI WA UTAMADUNI KATIKA CHUO CHA MAKUMIRA ARUSHA AUWAWA KINYAMA Reviewed by KUSAGANEWS on November 03, 2016 Rating: 5

No comments: