Mtu mmoja ambaye ni mfugaji ameuawa kikatili na kundi la
watu wenye hasira kali wa kijiji cha Kifone katika kata ya Mwimbi wilaya ya
Kalambo mkoani Rukwa, baada ya kutokea kutoelewana kati ya wakulima na
wafugaji.
Ukatili huo umetokea kufuatia kundi la Ngombe kuachiliwa
kuingia kwenye mashamba ya wakulima na kuharibu kiasi kikubwa cha mazao jambo
lilizua taharuki ndipo kupelekea kifo cha mfugaji huyo.
Akizungumza diwani wa
kata ya Mwimbi Claudio Mweupe, wamesema licha ya mfugaji huyo kuuawa kikatili
kwa kukatwa katwa na mapanga, lakini na mwenziwe naye Rehi Mwandu amejeruhiwa
vibaya baada ya kushambuliwa na kundi hilo la wakulima,
Mpaka sasa majeruhi amelazwa kwenye hospitali ya rufaa ya mkoa wa
Rukwa mjini Sumbawanga, huku msako mkali ukiendelea kuwatafuta watu wote
waliohusika na kitendo hicho cha kujichukulia sheria mkononi.
Mkuu wa wilaya ya Kalambo Julieth Binyura, akiongea kwenye
kijiji hicho cha Kifone akiwa ameongozana na kamati ya ulinzi na usalama ya
mkoa chini ya mwenyekiti wake Bw Zelote Steven, amesema tayari wameanza
kuwashikilia viongozi wa vijiji na vitongoji wanaoruhusu makundi ya Ngombe
kuingia kwenye maeneo yao.
MTU MMOJA AUWAWA KIKATILI KUTOKANA NA MGOGORO WA WAKULIMA NA WAFUGAJI MKOANI RUKWA
Reviewed by KUSAGANEWS
on
November 13, 2016
Rating:

No comments:
Post a Comment