![]() |
| Jaji kiongozi wa mahakama kuu ya Tanzania Ferdinand Wambali |
Jaji kiongozi wa mahakama kuu ya Tanzania Ferdinand Wambali amewataka mahakimu katika
ngazi zote hapa nchini kutoa maamuzi ya mashauri yanayofikishwa mbele yao kwa
kuzingatia viapo vya taaluma yao na ushahidi unaotolewa mahakamani ili waweze
kuheshimika ndani ya jamii.
Mheshimiwa Wambali ambaye yuko mkoani Kagera kwa ajili ya
ziara ya siku moja amesema mtumishi wa idara ya mahakama ataheshimika endapo
atatoa huduma nzuri kwa wananchi hivyo mewataka wafanye kazi yao kwa kujiamini,
kitaaluma na kwa uaminifu mkubwa.
Baadhi ya watendaji wa mahakama wamesema wameiomba idara ya
mahakama iwaondoe washauri wa baraza kwenye mfumo wa mahakama za mwanzo katika
kutoa maamuzi.
Naye mtendaji wa mahakama kuu Tanzania Solanus Nyimbi amesema
ufinyu wa bajeti ndio unakwamisha baadhi
ya mipango ya idara ya mahakama.
MAHAKIMU WATAKIWA KUFANYA KAZI KWA WELEDI ILI KUTENDA HAKI
Reviewed by KUSAGANEWS
on
November 13, 2016
Rating:
Reviewed by KUSAGANEWS
on
November 13, 2016
Rating:


No comments:
Post a Comment