|
Mkuu
wa Wilaya ya Ngorongoro Mhe. Rashid Mfaume Taka (kulia) akifunga Mkutano wa
hadahara uliofnyika katika Kata ya Digo Digo.
|
|
Katibu Tawala wa Mkoa wa Arusha Ndg. Richard
Kwitega akiwa na wananchi wake ambao anawachangia Fedha kwa ajili ya kujiunga
na Tika.
|
Wananchi wa Kata Pinyinyi, Wilaya ya Ngorongoro
wanasumbuliwa na ugonjwa wa ajabu wa kutapika damu kwa takribani miaka minne
sasa na hali hii imewasababisha wananchi hao kuwa na hofu na kukosa amani ya
kuendelea kuishi katika makazi yao.
Wakiwasilisha kero zao mbele ya Mkuu wa Mkoa wa Arusha
Mhe. Mrisho Gambo ambaye yuko katika ziara ya Kikazi kwenye Wilaya hiyo
wananchi hao wamesema mpaka sasa wananchi zaidi za ishirini wamefariki dunia
kutokana na ugonjwa huo ambao mpaka sasa hawafahamu kwamba ni ugonjwa gani.
“Ugonjwa huu ulianza tangu 2012 na mgonjwa huwa
anatapika damu kwa kipindi kirefu na baadae hufariki na sisi kama wananchi wa
Kijiji hiki tulishapeleka taarifa hizi kwa Halmashauri ya Wilaya na wakaja
mpaka hapa kijijini lakini ufumbuzi wa ugonjwa huu haujapatikana kutokana na
kutokua na majibu sahihi ya chanzo na aina ya ugonjwa huu” alisema Zakayo
Siranga mkazi wa Punyinyi.
Aliongeza kwa kusema kuwa wagonjwa wa aina hii wakienda kutibiwa
katika Hospital zetu hawaponi lakini kuna wachache waliokwenda Nchi jirani ya
Kenya kupata matibabu walipona sasa hatuelewi nini ambacho kimeshindikana
katika Hospital zetu tunaomba Serikali itusaidie.
Akijibu hoja hiyo Mganga Mkuu wa Wilaya ya Ngorongoro
Dr. Omary Sukari amethibitisha kuwepo kwa ugonjwa huu na alieleza jitihada
ambazo zimefanyika kutafuta ufumbuzi wa ugonjwa huu na kuwa wamekwisha chukua
sampuli ya damu na kupeleka kwenye Taasisi ya Utafiti Magonjwa wa magonjwa ya
Binadamu(NIMR) lakini mpaka sasa hawajapata majibu kutoka katika Taasisi hiyo.
Rc Gambo alimuagiza Mganga Mkuu wa Mkoa Dr. Frida Motiki
kutuma wataalamu ndani ya wiki hii wa kufanya tafiti ya ugonjwa huo hatari na
kupeleka tena sampuli hiyo NIMRI ili kupata taarifa sahihi na kutafuta ufumbuzi
wa haraka.
“Ugonjwa huu ni hatari sana na sisi kama Serikali
hatuwezi kukaa Kimya kwa sababu unagharimu uhai wa watu, kwa takwimu hiyo ya
watu 21 kufariki ni kitu cha kusikitisha sana hivyo nahitaji kupata ufumbuzi wa ugonjwa huu kupitia kwa
wataalamu wangu wa Afya”.
Kata ya Pinyinyi
haijawahi kutembelewa na Kiongozi wa Ngazi ya Mkoa kwa zaidi ya miaka
kumi sasa wananchi hao walitoa shukrani zao kwa Mkuu wa Mkoa Mhe. Gambo kwa kuanzia ziara yake katika Kata
hiyo na kueleza kwamba wanaona sasa wao ni sehemu ya wananchi halali wa Mkoa
huu kwa kuwa walikua wamesahaulika kwa kipindi kirufu na wana imani kero zao
sasa zitapata ufumbuzi wa haraka.
UGONJWA WA KUTISHA WAUA WATU 21 NGORONGORO
Reviewed by KUSAGANEWS
on
October 05, 2016
Rating:
Reviewed by KUSAGANEWS
on
October 05, 2016
Rating:



No comments:
Post a Comment