MCHINA APOTEZA MAISHA KATIKA BARABARA YA SAKINA -TENGERU WAKATI AKIWA KWENYE SHUGHULI.



Mfanyakazi wa kampuni ya Hanil Jiangsu inayoshirikisha wakorea na wachina inayofanya kazi ya upanuzi wa barabara ya kutoka Sakina-Tengeru  amefariki mara baada ya kukanyagwa na mtambo wa kushindilia barabara  unaofahamika kwa jina la Roller.

Kwa mujibu wa mashuhuda  wa tukio  hilo wanasema kifo  cha mfanyakazi huyo raia wa ya China  kimetokea pale ambapo mtambo huo wa barabara ulipokuwa ukirudi nyuma  ndipo  ulipomparamia raia huyo na kumkanyaga.

Kipindi hiki kilifika katika eneo la Kwa Mrefu mahali ambapo tukio hili limetokea na kushuhudia umati wa watu wakiwa eneo la hilo pamoja na vyombo vya ulinzi na usalama vikifanya juhudi za kumnasua chini ya mtambo huo ambapo alikuwa amekwama

Mara baada ya kunasuliwa  kwa mwili wa raia huyo aliyetambuliwa kwa  jina la Yao Sijiu mashuhuda wamezungumzia tukio hilo lililoleta taharuki kubwa mashuhuda hao wamesema kuwa ni Mara ya kwanza kwa tukio hilo kujitokeza tangu ujenzi huo wa barabara hiyo ulipoanza.

Kwa mujibu wa Jeshi la polisi mkoani Arusha kupitia taarifa ya maandishi limesema chanzo cha ajali ni uzembe wa opareta wa mtambo huo kutokuwa makini na kutochukua tahadhari ya usalama wa watu wengine waliopo eneo la kazi.

Mtuhumiwa anashikiliwa na jeshi la polisi  na mwili wa marehemu umehifadhiwa katika hospitali ya mkoa ya Mount Meru kwa uchunguzi wa daktari.
MCHINA APOTEZA MAISHA KATIKA BARABARA YA SAKINA -TENGERU WAKATI AKIWA KWENYE SHUGHULI. MCHINA APOTEZA MAISHA KATIKA BARABARA YA SAKINA -TENGERU WAKATI AKIWA KWENYE SHUGHULI. Reviewed by KUSAGANEWS on October 05, 2016 Rating: 5

No comments: