![]() |
|
Baadhi ya Watoto Wakifuatilia jambo
katika kongamano la watoto linaloendelea leo jijini Shinyanga
|
Kongamano la mtoto wa kike lililofanyika leo
mjini Shinyanga limeitaka serikali kuweka juhudi za makusudi kupinga vitendo
vya ukatili wa Kijinsia hasa kwa watoto wanaoozeshwa ndoa za utotoni kutoka kwa
wazazi na walezi wao.
Maadhimisho haya yanaendelea kufanyika mjini
Shinyanga ili kuungana na Nchi Wanachama wa Umoja wa Mataifa kuadhimisha Siku
ya Mtoto wa Kike inayoendelea kuadhimishwa Mkoani hapa ambayo kilele chake ni tarehe
11 Oktoba 2016.
Maadhimisho hayaufanyika kila mwaka ikiwa ni
mwitikio wa Azimio la Umoja huo lililopitishwa mwezi
Desemba mwaka 2011.
Akiongea
katika kongamano la watoto mkoani shinyanga Mkurugenzi wa Watoto Bi. Magereth
Mussai kutoka Wizara ya Afya, Maendeleo ya jamii, Jinsia, Wazee na Watoto
amelaani wale wote wanaoozesha watoto ambao wako katika umri wa kwenda shule
kwasababu ndoa za utotoni uwafanya watoto hawa kushindwa kufikia ndoto zao
ikiwemo haki ya kupata elimu ya juu.
Wakati
huo huo watoto wawili ambao hawakutaka majina yao kutajwa kwasababu ya kulinda
haki za watoto wametoa ushuhuda wao wa ni namna gani ndoa za kulazimishwa wakiwa
wadogo zilivyoelekea kukatiza ndoto yao kabla ya kuokolewa na shirika la AGAPE
kuwaokoa
na
kuwaendeleza kielimu.
Mmoja
wa Watoto hao ambaye jina limeifadhiwa amesema ndoa yake ya utotoni iligubikwa
na vipigo vya mara kwa mara kutoka kwa mme wake ambaye alimpatia ujauzito na
baadae kumtelekeza yeye na mtoto.
Alendelea
kusema kuwa inamuuma sana kama mlengwa kuwa mzazi na wakati huo kuwa mwanafunzi
anayesoma kwa msaada wa mashirika yasiyo ya kiserikali huku baadhi ya wazazi na
walezi wakiendeleza vitendo vya ukatili dhidi ya watoto.
Watoto
wao kwa pamoja wameitaka serikali na vyombo vya habari kuwekeza nguvu zao
kupinga vitendo vya ukatili wa kijinsia ikiwemo ndoa za utotoni ambazo zimekuwa
kikwazo kwa mtoto wa kike kufikia ndoto zake.
Kwa mujibu wa takwimu
za Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Idadi ya Watu (UNFPA),
inakadiriwa kuwa katika kipindi cha miaka kumi ijayo wasichana wapatao milioni
moja wanatarajiwa kuwa wameolewa katika umri wa chini ya miaka 18 duniani kote.
Maadhimisho ya Siku ya Kimataifa ya Mtoto wa Kike yaendelea Mkoani Shinyanga
Reviewed by KUSAGANEWS
on
October 08, 2016
Rating:
Reviewed by KUSAGANEWS
on
October 08, 2016
Rating:




No comments:
Post a Comment