Serikali Yakanusha Habari Zilizoandikwa na Gazeti la Kiingereza Kuwa Rais Magufuli Anaongoza Nchi Kwa Msukumo
SERIKALI
imekanusha habari zilizoandikwa na gazeti la Kiingereza linalotpka kila
wiki lililodai kuwa Rais Dk.John Magufuli anaongoza nchi kwa msukumo
licha ya kuonekana mzuri na kuwa taarifa hiyo imelenga kuupotosha umma.
Habari iliyoandikwa kwenye gazeti hilo ilikuwa na kichwa kilicho andikwa “Government by gesture, A President who looks good but governs impulsively”
Akizungumza
na waandishi wa habari Dar es Salaam leo mchana wakati akitoa ufafanuzi
wa habari hiyo Kaimu Mkurugenzi wa Idara Habari Maelezo, Zamarad
Kawawa alisema taarifa hiyo haikuwa na uzalendo na amewataka wanahabari
kuwa makini na habari zenye mlengo wa kupotosha taifa.
“Nawaombeni wanahabari wenzangu kuweni makini na taarifa zenye mlengo wa kupotosha umma” alisema Zamarad.
Akitoa ufafanuzi kuhusu suala la uchumi Meneja Uhusiano wa Kituo cha Uwekezaji Tanzania
(TIC), Daud Biganda alisema taarifa hiyo siyo sahihi na imelenga
kupotosha na inavuruga ukweli kwani Tangu Rais Dk.John Magufuli aingie
madarakani kwa kipindi cha kati ya mwezi Desemba 2015 na 2016, Kituo cha
Uwekezaji Tanzania
(TIC) kimeweza kuandikisha miradi ya uwekezaji ipatayo 551 yenye
thamani ya dola za kimarekani milioni 9,211.88 kati ya miradi hiyo
miradi 229 yenye asilimia 42 inamilikiwa na watanzania, miradi 215 yenye
asilimia 39 inamilikiwa na wageni na miradi 107 yenye asilimia 19
inamilikiwa kwa njia ya ubia kati ya watanzania na wageni.
Biganda
alisema kuwa miradi yote hiyo ya uwekezaji ilitarajiwa kuzalisha ajira
zipatazo 55,970 na kuleta matokeo mengine kwa watanzania na kuwa
imesajiliwa na TIC.
Serikali Yakanusha Habari Zilizoandikwa na Gazeti la Kiingereza Kuwa Rais Magufuli Anaongoza Nchi Kwa Msukumo
Reviewed by KUSAGANEWS
on
June 03, 2016
Rating:
Reviewed by KUSAGANEWS
on
June 03, 2016
Rating:


No comments:
Post a Comment