Mtu
mmoja ameuawa na tembo wengine kadhaa wamejeruhiwa katika mapambano kati
ya wananchi na kundi la tembo yaliyotokea katika kijiji cha kitendeni
kata ya Irkaswa tarafa ya Endyment wilayani Longido mkoa wa Arusha.
Mkuu wa Wilaya ya Longido
Bw.Ernest Kahindi amesema katika mapambano hayo pia tembo mmoja ameuawa
na wengine sita wamejeruhiwa na kwamba hali katika eneo hilo sio shwari
na huenda kukawa na madhara makubwa zaidi.
Akizungumza wakati
anaelekea katika eneo la mapambano hayo yanayodaiwa kuanza mapema alfajiri
Bw.kahindi amesema hatua za awali za kutuliza hali hiyo zilikuwa zinaendelea
kwa ushirikano wa viongozi wa ngazi mbalimbali na watendaji wa idara za
wanyamapori zikiwemo za kuwaondoa tembo hao katika eneo hilo zoezi ambalo
licha ya kuwa gumu lilikuwa linaendelea vizuri.
Aidha Bw.Kahindi amesema
tofauti kati ya tembo hao na wananchi ilijitokeza baada ya wanyama hao kumuua
kijana mmoja wa jamii ya kifugaji na ndipo wananchi hao wakajikusanya na
kuanza kuwatafuta tembo hao na kuanza kupambana nao kutaka kulipiza kisasi
ambapo pia mwananchi mwingine mmoja amejeruhiwa vibaya na tembo zaidi ya
sita pia wamejerihiwa vibaya kwa kuchomwa mikuki na kupigwa kwa silaha
zingine za jadi.
Hata hivyo Bw.Kahindi
ambaye ameambatana na kamati ya ulinzi na usalama ya wilaya kuelekea eneo la
tukio amesema taarifa kamili ya tukio hilo na hatua zitakazochukuliwa
itatolewa baadaye japo ameendelea kuwaomba wananchi kuepuka kuchukua sheria
mkononi ikiwemo ya kuamua kupambana na wanyama ili kuepusha madhara zaidi
kutokea.
Asilimia kubwa ya eneo hilo
ambalo ni mapito ya wanyama kwa muda mrefu sasa limekuwa katika hekaheka kati
ya wananchi na wanyama hao hasa unapotekea uharibifu ukiwemo wa wanyama
kula mifugo ya wananchi ama kuua watu.
Mtu mmoja auawa na tembo wengine kadhaa kujeruhiwa mkoani Arusha.
Reviewed by KUSAGANEWS
on
April 09, 2016
Rating:
Reviewed by KUSAGANEWS
on
April 09, 2016
Rating:


No comments:
Post a Comment