Katika hali ya kusikitisha mtu mmoja aitwaye Juma Bakari mkazi wa kijiji cha Mkamba wilaya ya Kilombero amenusurika kifo na kujikuta akiwa hana miguu yote miwili mara baada ya kuvamiwa na watu wasio julikana ambapo walimshika na kumkata miguu kisha kuondoka nayo huku wakimtelekeza katika mashamba ya kiwanda cha miwa(ILOVO).
Akizungumza na GUMZO TZ kwa masikitiko makubwa wakatia akiwa amelazwa
katika Hospitali ya Mtakatifu Francisco iliyopo mji mdogo wa Ifakara, majeruhi
wa tukio hilo Juma Bakari ameeleza namna ambavyo alikumbwa na kadhia hiyo
wakatia akitoka kumsindikiza rafiki yake aliyejulikana kwa jina moja la Hamza
na kushambuliwa na watu hao.
Nao ndugu wa majeruhi huyo
akiwemo mkewe Basilisa Sprian wameeleza kusikitishwa na kitendo kibaya
alichofanyiwa ndugu yao huku wakiomba msaada wa hali na mali utakaosaidia
kuyanusuru maisha ya kijana huyo.
Kwa upande wake mganga wa
zamu wa hospitali hiyo amekiri kumpokea majeruhi huyo akiwa katika hali mbaya
huku Kamanda wa jeshi la Polisi mkoa wa Morogoro Ulirich Matei amethibitisha
kutokea kwatukio hilo ambapo amesema Jeshi hilo linaendelea na uchunguzi ili
kubaini chanzo cha tukio hilo.
Mtu mmoja anusurika kifo baada ya kuvamiwa na watu wasiojulikana na kumkata miguu Kilimanjaro.
Reviewed by KUSAGANEWS
on
April 09, 2016
Rating:
Reviewed by KUSAGANEWS
on
April 09, 2016
Rating:


No comments:
Post a Comment