MKUU WA MKOA WA ARUSHA ABAINI WATUMISHI HEWA WENGINE AMBAO WAMEONGEZEKA SASA KUTOKA 270 MPAKA 320



Idadi ya Watumishi hewa wameendelea kuongezeka mkoani arusha baada ya oparesheni inayoendelea kuwasaka hao katika maeneo mbalimbali ndani ya wilaya za mkoa wa arusha.

Akizungumza na GUMZO TZ mkuu wa mkoa wa Arusha Daudi Felix Ntibenda amesema kuwa idadi hiyo ya watumishi hewa imeongezeka kutoka watumishi hewa 270 mpaka 320 kufikia hivi sasa nab ado oparesheni ya kubaini wengine inaendelea.

“mpaka leo hii nimetuma kamati yangu maalum ya kushughulikia watumishi hewa na tunaendelea kuwabaini kila siku na tuko makini katika kuhkikisha tunawabaini wote na kuwashughulikia kwa uhakika”alisema

Ntibenda ameongeza kwamba wanapokamatwa watumishi hewa na kubainika lazima walipe pesa zote walizo tumia na kasha sheria ifuate mkondo wake na kuwaburuza mahakamani haraka iwezekanavyo.

Na amesisitiza kwamba mtumishi hewa atakapobainika  atabanwa  mpaka aseme nani alimuajiri na kushughulikia na wote kuchukuliwa sheria zaidi na hili likiwa ni agizo maalum kutoka kwa raisi ambalo mpaka sasa linatekelezwa.

Mkoa wa Arusha mpaka sasa unaongoza kwa kufanya vizuri katika zoezi la kubaini watumishi hewa na kwa mujibu wa mkuu wa mkoa amesema huenda wakaongezeka zaidi kwasababu zoezi hilo bado ni endelevu.

“Na mpaka sasa watumishi hewa hao wanahaha na wameshanza kurudisha fedha na wengine wameshahama hata wizara zao nawengine kukimbia lakini tutawabaini tu”alisema

MKUU WA MKOA WA ARUSHA ABAINI WATUMISHI HEWA WENGINE AMBAO WAMEONGEZEKA SASA KUTOKA 270 MPAKA 320 MKUU WA MKOA WA ARUSHA ABAINI WATUMISHI HEWA WENGINE AMBAO WAMEONGEZEKA SASA KUTOKA 270 MPAKA 320 Reviewed by KUSAGANEWS on April 13, 2016 Rating: 5

No comments: