SHEHE MKUU WA TANZANIA AFARIKI DUNIA


 Habari zilizotufikia hivi punde zinaarifu kuwa Mufti Mkuu wa Tanzania, Sheikh Shaaban Issa Simba amefariki dunia.

Akidhibitisha kutokea kwa kifo hicho Shehe Mkuu wa mkoa wa Dar es salaam Sheikh Alhadi Mussa Salim amesema Mufti amefikwa na umauti hii leo asubuhi katika Hospitali ya TMJ alikokuwa amelazwa kwa matibabu.

"Ni kweli Mufti Mkuu wa Tanzania, Sheikh Shaaban Issa Simba amefariki hii leo asubuhi kwa maradhi ya sukari na presha," alisema kwa ufupi Sheikh Alhhadi.

Mwili wa marehemu umehifadhiwa katika Hospitali ya Jeshi Lugalo na unataraji kusafirishwa kesho kwenda  mkoani Shinyanga  kwaajili ya maziko. 
Father Kidevu Blog inaungana na waislamu wote nchini katika maombolezo na inawapa pole Familia yake, ndugu jamaa na marafiki na wailsamu wote ndani na nje ya Tanzania. 


INNA LILLAH WA INNA ILLAHI RAJIUN.

Hakika sisi sote ni wa Mwenyezi Mungu. 

SALAMU ZA RAMBI RAMBI 

SALAMU za rambi rambi kufuatia msiba huo mzito zimeanza kutoklewa ambapo Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Mheshimiwa Dkt. Fenella Mukangara (Mb.) ametuma salamu za rambirambi kwa Baraza Kuu la Waislamu Nchini (BAKWATA) na Waislamu wote nchini kufuatia kifo cha Sheikh Mkuu wa Tanzania Mufti Shaaban Issa Bin Simba kilichotokea Jumatatu, tarehe Juni 15,2015 katika hospitali ya TMJ Jijini Dar es Salaam alipokuwa anatibiwa.


Katika salamu hizo, Mhe. Mukangara amesema kuwa ni jambo la kusikitisha kumpoteza kiongozi huyo ambaye bado Taifa lilikuwa likimuhitaji hasa katika kipindi hiki cha kuelekea uchaguzi Mkuu wa mwezi  Oktoba mwaka huu. 
Waziri huyo ameongeza kuwa Mufti atakumbukwa kwa upole  , unyenyekevu wake na kutopenda makuu,wakati wa uhai wake marehemu alikuwa tayari kumsikiliza kila mtu bila kujali dini au kabila lake.
“Nimepokea kwa huzuni nyingi taarifa ya kifo cha Sheikh Mkuu wa Tanzania Mufti Shaaban Issa Bin Simba ambaye alikuwa Kiongozi anayeshirikiana vizuri na viongozi wote wa serikali na vyama mbalimbali katika kuhakikisha Watanzania wanaendelea kuwa wamoja” amesema .
Amesema Waziri Mukangara: “Nakutumia salamu zangu za rambirambi wewe Katibu Mkuu, BAKWATA na waislamu wote nchini na naungana nanyi katika kuomboleza msiba huu mkubwa katika nchi yetu.
Aidha, kupitia BAKWATA, natuma salamu za dhati ya moyo wangu kwa familia ya marehemu kwa kumpoteza mpendwa wao. Napenda wajue kuwa msiba wao ni msiba wangu. Pia, naungana nao katika kumwomba Mwenyezi Mungu, Mwingi wa Rehema aiweke pema peponi roho ya marehemu … Amina.”
SHEHE MKUU WA TANZANIA AFARIKI DUNIA SHEHE MKUU WA TANZANIA AFARIKI DUNIA Reviewed by KUSAGANEWS on June 15, 2015 Rating: 5

No comments: