Vurugu hizo zilitokea saa 5:30 asubuhi, mara baada ya Lema kuingia eneo hilo akitembelea vituo vya kuandikisha wapiga kura kuangalia hali halisi.
Alipofika kwenye kituo hicho alikuta mmoja wa Polisi akiwa amevaa kiraia (Jina halikupatikana mara moja), akiwa na daftari dogo akiorodhesha majina ya wapiga kura kwa lengo la kupunguza foleni.
Akizungumza na wananchi huku Lema akiwa amezungukwa na askari polisi, alisema huo sio utaratibu wa kufanywa na polisi na hata Tume hairuhusu Polisi kufanya kazi hiyo bali kulinda amani tu.
Hata hivyo, Mkuu wa Kituo Kikuu cha Polisi cha Arusha, Thomas Maleko, akimtuliza hasira Lema akisema wao wanafanya kazi hiyo, ili kuwapunguzia adha wananchi ambao wanafika kituoni saa 9:00 usiku, hadi siku ya pili wanakaa kutwa nzima bila kupata fursa ya kuingia chumba cha kujiandikisha.\
Alisema kutokana na hali hiyo, ndipo Polisi walipoamua kuandikisha watu kwa makubaliano na waandikishwaji wenyewe, ili waondoke nyumbani wakafanye kazi zingine na kesho yake wakirejea wanapata fursa hiyo.
“Hawa watu hata wakikaa hapa hawawezi kuingia ndani ya chumba husika, maana kuna kompyuta moja tu, hivyo wanapigwa na jua, hivyo utaratibu huu sisi tumeona ni mzuri, tunaandika jina la mtu kisha tunamruhusu aende nyumbani hadi kesho aje anaingia ili kupata kitambulisho,” alisema.
Hata hivyo, licha ya maelezo ya polisi, Lema hakukubaliana nayo na kuwasiliana na Mkurugenzi wa Jiji la Arusha, Juma Idd ambaye alimtuma Mjumbe wa Tume ya Uchaguzi, ambaye naye hakutaka kuzungumza chochote na waandishi wa habari na pia hakutaka kutaja jina lake.
MBUNGE WA JIMBO LA ARUSHA MJINI ATETEA BIOMETRIC VOTERS REGISTRATION KWA KUPAMBANA NA POLISI
Reviewed by KUSAGANEWS
on
June 18, 2015
Rating:
No comments:
Post a Comment