ALBINO WANA HAKI YA KUISHI KAMA WEWE

 Albino ni watu wenye ulemavu wa ngozi, wanaogopa mwanga wa jua kwani kutokana na ngozi yao ni rahisi sana kuungua na jua, pia uwezo wao wa kuona ni dhaifu, tofauti na mtu wa kawaida. Watu hawa huitwa "watoto wa mwezi". Kwa sababu mwanga mkali wa jua unaharibu ngozi yao, wanakuwa huru zaidi nyakati za jioni wakati mbalamwezi iko angani. Katika muda mrefu uliopita, watu hao wanabaguliwa na kuishi katika hali dhalili, huku wakitawaliwa na woga kutokana na ngozi yao kuwa tofauti. Wengi wetu hatujui mengi kuhusu ugonjwa wa albino, hata baadhi yetu tuna wasiwasi kuwa ugonjwa huo unaweza kuambukizwa.

Tarehe 13 mwezi huu, ni maadhimisho ya kwanza ya Siku ya Kimataifa ya Albino. Kwa Albino, siku hiyo ni maalum kwao, na wanaichukulia kama sikukuu yao. Hivi karibuni waandishi wetu habari wafanya mahojiano na Albino hapa China, Tanzania na Kenya, kwa lengo la kutaka kuelewa maisha yao pamoja na matumaini yao. Tunatumai watu wengi zaidi wanapata uelewa kuhusu Albino, kuondoa dhana potofu juu yao, na kutoa misaada mikubwa zaidi kwao, hususan watoto. Na kama nilivyowajulisha awali, kipindi cha leo ni cha kwanza na kinaitwa "malaika wanaoanguka kwenye Ziwa Kuu".
Albino inasababishwa na upungufu wa upungufu wa madini ya melanin katika ngozi na viungo mbalimbali kama nywele, ambao unarithishwa kizazi hata kizazi, hasa kwa watu wenye undugu wa karibu zaidi. Kutokana na rangi tofauti ya nywele na ngozi, Albino huchukuliwa kama watu waoatisha na wanatoka katika familia ya mashetani wanaovaa nguo nyeupe, na wana uwezo mkubwa sana. Watu huwa na chuki dhidi yao. Nchini Tanzania, kutokana na ndoa kati ya ndugu wa karibu na hali duni ya matibabu, miongoni mwa watu 1400, mmoja ni albino kwa wastani, kiasi ambacho ni kikubwa zaidi kuliko kiasi cha 1/20000 katika nchi zilizoendelea.
"Watu wanadhani sisi hatutakufa, wanatuita 'Zeru Zeru', maana mzimu."
Mbali na hayo, katika nchi nyingi za Afrika kuna msemo kuwa, kwa kupitia voodoo, kunywa dawa za kichawi zinazotengenezwa na viungo vya Albino zitampatia mtu utajiri, mamlaka na mafanikio, hata kutibu magonjwa yoyote. Hivyo baadhi ya wahalifu wanavutiwa na manufaa makubwa kwenye "sekta hiyo", na kuwatafuta kwa udi na uvumba maalbino. Uhalifu wa kuwaua na kutumia viungo vya albino unatokea mara kwa mara. Biashara ya magendo ya viungo vya albino ni tatizo linalojirudia mara kwa mara, hata baadhi ya jamaa maskini wanawauza watoto wao wenye albino.
"Taarifa ya habari ya leo, msichana mmmoja albino ametekwa na juhudi zinafanyika kupata ushahidi husika ili kumuokoa msichana huyo. Lakini jambo linalotia wasiwasi ni kuwa, kesi nyingi kuhusu mauaji ya Albino zinatokea hivi karibuni."
Kama alivyosema askari, Albino wengi hutekwa nyara nchini Tanzania, na uwezekano kwa watu hao walitekwa nyara kupatikana ni mdogo sana.
"Hii ni wilaya ya tatu katika mkoa huu inayoongoza kwa kukata viungo vya albino, Geita inaongoza, ikifuatiwa na Magu, zinafuatiwa na Misungwi, na Kwimba. Tupambane nalo na iwe ndio mara ya mwisho"
Lakini kesi hiyo inayoogopesha watu ni moja kati ya kesi nyingi zinazofanana katika sehemu hiyo. Mwanza ambao ni mji mkubwa wa pili nchini Tanzania uko kaskazini magharibi mwa nchi hiyo. Mwenyekiti wa shirikisho la albino la Mwanza Alfred Kapole anadondokwa na machozi anapotuzungumzia kesi hizo dhidi ya watoto albino.
"Tarehe 27 mwezi Desemba mwaka jana kuna mtoto aitwaye Pendo Mwameli wa kijiji cha Ndami mkoa wa Mwanza aliibiwa na kutokomea kabisa kusikojulikana hadi sasa, na mpaka sasa hatutajua yuko wapi. Mwezi uliofuata mtoto mwingine Yohana bahati mwenye umri wa mwaka mmoja na nusu naye vilevile aliporwa kwenye mikono ya mama yake na kukimbia naye na baadaye kukatwa viungo vya mikono na miguu na kuachwa mwili wake. Lakini vilevile mama yake alijeruhiwa na kulazwa hospitali na anaendelea na matibabu hadi sasa."
Hali hiyo ya mauaji ya mara kwa mara imesababisha albino pamoja na jamaa zao wanaishi kwa hofu kila siku. Kwa mujibu wa takwimu husika kutoka shirikisho la kimataifa linalosimamia haki za albino, mwaka uliopita, katika nchi 28 za Afrika, idadi iliyothibitishwa ya mauaji ya albino ilifikia 129, na wengine 181 wamejeruhiwa, wengi zaidi ni watoto.
"Hivi majuzi mama wa mtoto mmoja aitwaye Selina Magda alitumiwa ujumbe wa kutishiwa na kuambiwa kuanzia sasa mtoto wako tutamuuwa na kunyofoa viungo vyake, kwa hiyo baada ya kutumiwa ujumbe huo alinipigia simu akiwa polisi kituo cha Magu. Baadaye nilienda Magi kufuatilia nikaonana na viongozi wote wa serikali ili kuona usalama wa huyo binti mwenye umri wa miaka 23. Kwa hiyo kwa wastani hali katika kanda ya ziwa imekuwa mbaya sana na watu kwa sasa wanaishi kwa hofu. Tunaishi kwa hofu kwasababu na mimi pia ni albino"
Mji wa Mwanza uko karibu na Ziwa Victoria ambalo ni ziwa kubwa zaidi barani Afrika. Wavuvi wengi wa huko wanaamani kuwa wakiweka nywele za albino kwenye nyavu zao, watapata samaki wengi. Hivyo albino, hususan watoto wanaishi kwa wasiwasi.
"Mauaji ya albino yanatokea hapa na pale, ni mbaya sana, hususan katika sehemu hii, nasikia wanawaua albino kama wanaua kuku."
Familia nyingi zenye watoto albino zinafanya kila linalowezekana kuwalea, kwani watoto hao ni malaika na wanapendeza machoni mwa wazazi wao. Lakini watoto hao siku zote wanafuatwa kama wanaowindwa, maana kufumba na kufumbua macho, wanawezekana kuibwa na kuuawa. Hii inawafanya wazazi wao kuwa na uchungu sana.
"Alipozaliwa, nilishangaa sana kumwona ni albino. Nini kimetokea kwa mtoto huyu? Mtoto huyo anatofautiana kabisa na jamaa zangu. Lakini nasikia yeye ni malaika aliyeletewa na Muungu. Niliamua kumlea na kumtunza vizuri. Lakini alipokuwa na umri wa miaka 10…"
"Lakini aliuawa, aliuawa kama mnyama. Watu walimfuatilia kwa kipindi fulani, mwisho walimchukua"
Kama ilivyo Tanzania, nchini Kenya, ingawa imani za kishirikina hazijaenea sana sehemu za mijini, lakini kesi za mauaji ya albino pia zinatokea mara kwa mara. Kutokana na uelewa duni kuhusu Albino, hali ya maisha ya watoto albimo vilevile inawatia watu wasiwasi. Baadhi ya baba wa watoto hao wanadhani wake wao wana mahusiano ya kimapenzi na wazungu, basi watoto wana ngozi nyeupe, hivyo hawatunzi watoto wao.Takwimu zinaonyesha kuwa, nchini Kenya asilimia 90 ya watoto albino wanatunzwa na mama zao pekee. Aidha kutokana na ubaguzi, Albino wengi wanaishi kwa kujitenga au kukimbia nyumba zao. Kuna shule moja maalum mjini Mombasa, ambayo watoto wengi albino wanajumuika na kuishi kwa pamoja.
"Sisi ni wanafunzi wa shule ya Likoni. Tunasema, tulinde sisi watoto, sisi ni future of jamii. Tunafanana na watoto wengine. Tunastahili kupewa nafasi. Tunaweza."
Jacinta Mkanyika anasoma darasa la sita kwenye shule hiyo, anatumai sana kuisaidia familia yake baada ya kuhitimu elimu yake.
"Baba na mama yangu wakiwa wazee, wakiwa na ugonjwa, nitawatunza, nitawapelekea hospitali. Nitawajengea nyumba kubwa na kuwapikia vyakula tamu. Kweli sisi hatuna tofauti kubwa na watoto wengine. Sisi tunasoma, tunakula, tunacheza, tunafanya kazi, tunajisaidia. Lakini wakati fulani tulishinda watoto wa kawaida kwenye mitihani. Nataka kuwambia wenzangu kuwa, tuishi kwa furaha."

Tamasha Nassoro ni mama wa watoto wawili albino. Anasema wazazi wanapaswa kuwaona kama watoto wengine, hawawezi kuwafungia nyumbani au shuleni, wanatakiwa kupewa nafasi ya kuwasiliana na watoto wengine na jamii kwa ujumla.
"Hatuweza kuwatenganisha watoto wa albino, tunapaswa kuwaingiza watoto wenzao, na kuwafundisha ufundi. Kama walivyosema wazazi wengine, nafanya hivyo vilevile. Wana poor eyesight, basi tuwasaidie kuwaambia wafanye hivi wafanye vile. Tukiwa wazazi, tunabidi kuwa na uangalifu juu ya watoto wetu, wakicheza nje, wakirudi nyumbani, tunabidi kuwa na uangalifu."
Samy Kiranga ni mwalimu wa hesabu wa darasa la sita. Anawafundisha watoto, na vilevile ana jukumu la kuwafundisha maisha ya kawaida pamoja na afya ya mwili na saikolojia.
"Muhimu zaidi ni kuwa, watoto wanapaswa kujua kulinda macho yao. Tunapendekeza wafanya nini, ili wajue namna ya kujilinda. Vilevile nataka kuwaambia wengine, tusibagua watoto wa albino. Tuwape nafasi, wao ni watoto, wakifanya juhudi, watatoa michangoa yao kwa jamii."
Jane mutunga naye pia ni mwalimu mwingine katika shule hiyo. Anasema, vitabu na vifaa vya masomo kwa watoto albino ni maalum, anaona fahari kwa wanafunzi wake.
"Baadhi ya watoto wa albino wanaochapa kazi,hata masomo yao ni mazuri zaidi kuliko watoto wale wa kawaida.Hii itawafanya wajiamini zaidi, na kutambua 'kumbe sisi sio inferior to wengine'. Na wakihitimu kutoka shule na kuingia jamii, watatambua wao ndio muhimu katika jamii."
Kama mwalimu huyo alivyosema, kwa upande wa matibabu, albino hawana tofauti na watu wa kawaida isipokuwa rangi ya ngozi, nywele na uwezo wa kuona, viungo vyao haviwezi kutibu magonjwa. Barani Afrika, maelfu ya albino wanahitaji kulindwa, na elimu kuhusu Albino inatakiwa kuenezwa. Ndio maana mwezi Oktoba mwaka jana, Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa lilitangaza kuwa tarehe 13 mwezi Juni kila mwaka ni Siku ya Kimataifa ya Albino, na lilitoa mwito wa kuongeza uelewa kuhusu albino na kuwasaidia. Jambo hili limewafanya albino wapate tumaini jipya la maisha.
ALBINO WANA HAKI YA KUISHI KAMA WEWE ALBINO WANA HAKI YA KUISHI KAMA WEWE Reviewed by KUSAGANEWS on June 15, 2015 Rating: 5

No comments: