Hatimaye rais wa Zanzibar na mwenyekiti wa baraza la mapinduiz Dr Ali
Mohamed Shein amechukua fomu ya kutaka urais wa Zanzibar kwa tiketi ya
CCM huku akitamba hakuna mgombea wa upinzani yeyote anayempa hofu
.
.
Dr Shein akifuatana na mke wake mama Mwanamwema na baadhi ya
wanfamilia waliofika afisi kuu ya CCM kiswandui na kulakiwa na umati
mkubwa wa wana CCM waliofika kumuunga mkono na kukabidhiwa fomu hizo na
naibu katibu mkuu wa CCM Zanzibar Vuai Ali Vuai huku akilipiwa ada ya
shlingi milioni moja na mkewe.
Baadaye alizungumza na viongozi wa ngazi mbalimbali wa chama wa
mikoa yote ya Zanzibar ambapo mbali ya kuwashukuru na kuwahidi
kuwatumkia kwa nguvo zote wazanzibari kwa misingi ya sheria na katiba na
kulinda mapinduzi na muungnao na baadaye alizungumza na waandishi wa
habri ambapo amemsmea hawaogopi na wala hatishiki na wagombea urais
waznazibar kutoka vyama vyengine kwa vile wote anawaweza.
Akitoa sababu za msingi zilizofanya agombea nafasi hiyo ya uris kwa
mara ya pili Dr Shein amesema hawezi kuondoka sasa kwa vile malengo
yaserikali yake aliyoyaweka hayajamalizika hivyo anataka kipindi cha
pili ili afikie huko na kuwaachia wazanziabri mustakabali mzuri wa nchi
ikiwemo masuala ya mafuta na gesi na uchumi.
Dr Shein ambaye anatarajiwa kuwa mgombea pekee wa CCM anakuwa
mgombea wa sita kutangaza kuwania urais wa Zanzibar wengine waliotangaza
nia ni Maalim Seif Sharrif Hamad-CUF, Juma Ali Khatibu -TADEA, Saiid
Soud -AFP, Hamad Rashid-ADC na mgombea wa Jahazi Asilia.
Dr Ali Mohamed Shein achukua fomu kutetea nafasi yake Zanzibar.
Reviewed by KUSAGANEWS
on
June 18, 2015
Rating:
No comments:
Post a Comment