Ni jambo la
kushangaza sana kwa waimbaji wa nyimbo za injili mana lengo hasa kuimba nini?
Kuimba mziki wa injili sasa ni ajira? au ni wito kutoka kwa Mungu?
kwasababu wasikilizaji wanategemea kupata ujumbe kwa
kubariki watu,kugusa nafsi za watu,na pia kuponya watu na kupata matumaini ya
kuishi tena kutokana na jumbe hizo muhimu
Jambo la kushangaza kwasasa waimbaji wa injili wapo badala ya pesa
huweziona muimbaji wa nyimbo za injili wapo kwenye matamasha bure wanachotaka
ni pesa na tena kwa ushindani mkubwa.
Eeeeeeeeeeeeeehh Mungu tusaidie katika hili mana hata Biblia
zimeeleza wazi kwamba tukusifu kwa moyo na tufanye kazi kwa moyo hivyo mambo
haya yanatokea wapi oooooooooh Yesu tuwezeshe
Safari ya uimbaji bado inaendelea waimbaji hawahawa wa
injili ndiyo mlio na skendo mbaya hata za kumuabisha Mungu ndoa za waimbaji
hawa zimeharibika kisa uimbaji wa injili
Waimbaji wapo hivihwa baadhi yao
Mtu : Halooo habari yako BwanaYesu asifiwe
samahani sisi ni kanisa ambalo tunaomba uje Arusha kuna tamasha sasa tunaomba
ujumuike nasi karibu sana katika tamasha letu tunakutegemea
Mwimbaji:Amina
mpendwaa ok kuna kazi kidogo nafanya lakini nitakuja ila nitumieni kwanza
shilingi laki mbili niangalie kwamba ntakuja katika tamasha lenu au la. HIZO ndiyo kauli za baadgi ya wana gospel.
Je huyu mwimbaji wa injili anataka atumiwe kwanza sh laki
mbili unaona lakini utamkuta mwimbaji huyu anasema anataka Mungu amuinue awe
mwimbaji bora duniani.
Ukweli wa mambo usemwe kwasasa waimbaji wengi wako badala ya
pesa ahahahahahahah mwimbaji mmoja maarufu sana hapa nchini Tanzania
ameshasahau nini anafanya na kutunga nyimbo za kisiasa kusifu mtu sasa nauliza
ni Mungu tutamsifu au ni viongozi wa kisiasa?
Waimbaji hebu
angalieni mtajibu siku ya mwisho kuhusiana na kazi zenu na tabia za waimbaji hawa wa injili ni watu
wenye Dharau,kuona waimbaji chipukizi hawana maana na kujiona wao ndiyo bora
zaidi lakini ukweli wa mambo upo nyie mnaabisha kabisa kwa baadhi yenu.
Lakini ashukuriwe Mungu kwa wale walioitwa kwa ajili ya kazi yake Mungu
na hawa hawapo badala aya pesa wanatumia kipawa hiki kuinua wengine.
Ila kwa skendo hamjambo na hamjui fikra zilizopo kwa watu
mana nyie ni barua ya kusomeka na watu ila
sasa barua hizi mmezichafua hata zimejaa matope
Je?nanyi wachungaji
baadhi yenu mbona mnachangia kuwapotosha na kuwapa kiburi waimbaji hawa ?Skendo
zenu zimewshika doria kila kona sasa sina budi kuuliza wote mmeitwa mana wapo
walioitwa na wakatii sauti ya Mungu
unyenyekevu na hekima ndo jambo la msingi katika huduma zenu mana
mafundisho ya wachungaji mengi katika masinagogi ni kuhusu kutoa sadaka je?hizi
sadaka ndiyo mtaji tena na kuweka kiwango cha pesa nilienda kanisa moja mahali
flani mchungaji akaseama mimi sitaki sh elfu moja kwenye kanisa langu sasa
nikapata wasiwasi mkubwa juu ya shilingi hizi hivyo kulingana na hili
mmewafunza waimbaji kudai peasa wakati wanaalikwa kwenye matamasha
Je?majibu
yatapatikana vipi mmewadanganya watu kwa kusema mnaponya ni lini mchungaji
aliponya mtu bila Mungu aliyewapa pumzi?
,,,Napenda kutumia
mfano wa mwimbaji huyu ambaye pia ni mwimbaji wa gospel si mwingine ni Past Abiud Misholi popote ulipo Baba Mungu akupe maisha mana kazi anayoifanya
huyu baba ni ya kuigwa na hawa ndiyo watumishi walioitwa na Mungu siyo kujiita ,,,
Mhmhmhmhmhmh?Nasikia utamu wa Yesu ni
kweli upo lakini je upo kwenu nyie mnaosema upo mbona ninyi ndiyo wa kwanza
kuuharibu utamu huu wa Yesu?
Waimbaji wa injili
mnatofautiana kidogo sana na wasanii wetu wa kibongo au bongo flava kwasababu
jinsi mnbavyokata mauno kanisani hamna tofauti na Diamond akiwa jukwaani na
dancer wake.
Maneno tu ndiyo
yanawatofautisha tu lakini mengine sijaona.Sasa swali langu mnataka magorofa tu
na kuwapa pesa mnapo waambia watu wawape pesa kabla ya ya kufanya kazi?
Mimi ni mwimbaji wa Gospel lakini nimefunguka kusema haya
nab ado nitayasema tuuuu mana tumeacha njia ya Bwana tukafuata yetu wenyewe.
Lakini kamwe ukweli nitauseama na kupasua majibu ya siku
nyingi ambayo hayakuwa na dawa aya kutibu
Itaendeleaaa…………………………………..
UKWELI KUHUSU MZIKI WA INJILI HAPA TANZANIA IMEKUWA KIPATO KWA WAIMBAJI NA UKWELI WA MAMBO
Reviewed by KUSAGANEWS
on
May 13, 2015
Rating:
No comments:
Post a Comment