Itakumbukwa kwamba mpaka kufikia Januari mwaka jana Dola ilikuwa ikibadilishwa kwa Sh1,630 na ilikuwa ikiporomoka taratibu mpaka kufika Sh1,850 na Sh1,900 ilipofika Februari mwaka huu. Kwa sasa ni zaidi ya Sh2,000.
Kuna sababu mbalimbali zinasababisha kuporomoka kwa thamani ya shilingi.
Zipo sababu za kiuchumi ambazo pia zimegawanyika
kwa kigezo cha ndani na za nje. Vilevile zipo sababu za sera na
usimamizi wa sheria za nchi kuhusu masuala ya kifedha.
Sababu ya kwanza ambayo husababisha kushuka kwa thamani ya fedha ya nchini yoyote ni urari wa kibiashara (balance of trade).
Katika urari wa biashara, kinachoangaliwa ni namna
nchi inavyoweza kuuza vitu nje pia inavyoagiza vitu kutoka nchi za nje.
Kama nchi inatumia bidhaa nyingi za nje kuliko zile za ndani na inauza
vitu nje kwa kiasi kidogo kuliko inavyoviagiza basi thamani ya fedha ya
nchi hiyo lazima ishuke kwa kasi.
Kwa Tanzania bidhaa nyingi tunazozitumia ni za nje
hivyo tunahitaji zaidi Dola ili tuweze kununua bidhaa hizo katika soko
la dunia. Hii inapekea hitaji la shilingi liwe dogo ikilinganishwa na
hitaji la Dola hivyo thamani ya Dola inakuwa juu kuliko ya Shilingi ya
Tanzania.
Suala jingine linaloweza kuathiri thamani ya fedha
ya nchi yoyote ni masuala ya uwekezaji kutoka nje yaani Foreign Direct
Investment (FDI).
Uwekezaji wa nje ukiongezeka kwa kiasi kubwa
husababisha thamani ya fedha ya nchi husika kupanda kwa sababu hitaji
lake linakuwa kubwa kwa wawekezaji ambao wanaendesha miradi yao kwa
gharama kubwa kwa fedha ya nchi husika.
Hatujapata bado tamko la serikali ama takwimu
zozote zinazoonyesha kama uwekezaji kutoka nje umepungua ama wawekezaji
wamepunguza mitaji lakini ni moja kati ya sababu ambazo za kushuka ama
kupanda kwa thamani ya fedha katika nchi husika.
Thamani ya fedha inaweza pia kuathiriwa na
uwekezaji ambao unavuka mipaka ya nchi na sekta mbalimbali kwa lugha ya
kimombo; portfolio Investment.
Hii ni aina ya uwekezaji ambao huendeshwa kwa
mitaji ya hisa kwa watu kutoka katika mataifa mbalimbali kwa mfano mtu
anaweza kuwa ni Mtanzania lakini akawa anahisa katika kampuni ya
Uingereza.
Kukiwapo na portifolio investment nyingi hapa
kwetu hisa zake zitakuwa zinauzwa kwa shilingi hivyo watu wa mataifa
mbalimbali watahitaji kuinunua ili waweze kuwekeza.
Nini kinaporomosha shilingi ya Tanzania?
Reviewed by KUSAGANEWS
on
May 07, 2015
Rating:
No comments:
Post a Comment