Mkuu wa Mkoa wa Arusha , Paul Makonda amewaomba Wenyeviti wa Bodi na watendaji Wakuu na Taasisi za Umma kuchangamkia Fursa ya uwekezaji katika utalii wa matibabu kwa kujenga hospitali kubwa itakayokidhi mahitaji ya wageni mbalimbali wanaotembelea jiji hilo.
Akizungumza katika kikao Kazi cha wenyeviti wa Bodi na Watendaji wa Taasisi za Umma kilichohudhuriwa na Rais Samia Suluhu Hassan ,Makonda amesema matamanio ya Mkoa wa Arusha ni kuwa na Hospitali kubwa yenye madaktari kutoka mataifa tofauti na mbalimbali.
TUNATAMANI KUJENGEWA HOSPITALI KUBWA ARUSHA -MAKONDA.
Reviewed by KUSAGANEWS
on
August 28, 2024
Rating:
Reviewed by KUSAGANEWS
on
August 28, 2024
Rating:


No comments:
Post a Comment