KESI YA DOKTA PIMA NA WENZAKE BADO MAMBO MAGUMU WARIDISHWA MAGEREZA

Mawakili wa upande wa utetezi katika kesi ya uhujumu uchumi namba ya  mwaka 2022 inayomkabili aliyekuwa Mkurugenzi wa Jiji la Arusha Dakta John Pima na wenzake wawili wameuomba upande wa mashtaka kuharakisha upelelezi ili washtakiwa waweze kupata haki zao.

Mbali na Dakta Pima wengine katika shauri hilo ni aliyekuwa Mkuu wa Idara ya mipango na uchumi,Innocent Maduhu na aliyekuwa Mkuu wa idara ya fedha katika halamshauri hiyo,Mariam Mshana.

Shauri hilo ambalo lilipangwa leo kwa ajili ya kutajwa ambapo wakili wa Jamhuri Upendo Shemkole aliiambia mahakama kuwa upelelezi wa shauri hilo bado haujakamilika hivyo wanaomba tarehe nyingine kwa ajili ya kutajwa .

 Wakili wa utetezi Sabato Ngogo aliiomba upande mashtaka kuharakisha upelelezi huo ili washtakiwa waweze kupata haki yao na kama upelelezi unawasumbua waliondoe shitaka.

 Katika kesi nyingine ya uhujumu uchumi namba 3 inayomkabili Dakta Pima na wenzake watatu ambao ni Mshana,Maduhu na Nuru Ginana aliyekuwa mchumi wa jiji hilo,washitakiwa hao walishindwa kusomewa maelezo ya awali katika kesi hiyo.

 Wakili Upendo aliieleza mahakama kuwa shauri lilipangwa kwa ajili ya kuwasomea mwashitakiwa hao amelezo ya awali ila wanaomba kupangiwa tarehe nyingine bila kutoa sababu yoyote.

 Baada ya maelezo hayo,Wakili Sabato aliieleza mahakama kuwa leo ni mara ya tatu maelezo hayo kushindwa kusomwa huku kukiwa hakujatajwa sababu yoyote wakati walishasema upelelezi umekamilika.

 Wakili huyo aliomba mahakama iangalie mshitakiwa wa pili(Mariam) ana mtoto mdogo na kuwa watuhumiwa hao wanateseka na kuomba mahakama itoe amri kuwa tarehe itakayopangwa maelezo hayo yaweze kusomwa.

 Wakili wa jamhuri  alisema amesikia hoja na hakusema awali kwa kuwa maelezo hayo hayapo  tayari na katika tarehe inayotajwa watafanyia kazi ili kesi iweze kuendelea.

 Katika kesi nyingine ya uhujumu uchumi namba 4/2022 inayomkabili Dakta Pima,Mariam,Madumu na Alex Daniel,ambayo pia ilipangwa kwa ajili ya kusomewa maelezo ya awali,ilishindwa kuendelea baada ya jamhuri kueleza kuwa maelezo hayo hayapo tayari.

 Wakili Sabato aliomba washitakiwa hao wasomewe mapema maelezo hayo ili haki iweze kutendeka kwa washitakiwa hao.

 Hakimu Mbelwa aliahirisha kesi zote tatu hadi Agosti 11 mwaka huu.

 

KESI YA DOKTA PIMA NA WENZAKE BADO MAMBO MAGUMU WARIDISHWA MAGEREZA KESI YA DOKTA PIMA NA WENZAKE BADO MAMBO MAGUMU WARIDISHWA MAGEREZA Reviewed by KUSAGANEWS on August 01, 2022 Rating: 5

No comments: