Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), kimeadhimia
kuyapuuzia maagizo ya Spika wa Bunge la Tanzania Job Ndugai, aliyewataka
Wabunge wote wa chama hicho ambao hawahudhurii vikao vya Bunge kwa sasa
kurudisha posho walizolipwa, ambapo kwa umoja wao wanadaiwa zaidi ya Milioni
110.
Taarifa
hiyo imetolewa leo Mei, 11, 2020 na Katibu Mkuu wa Chama hicho John Mnyika,
wakati akitoa taarifa ya maadhimio ya Kamati Kuu ya chama hicho, ambapo pamoja
na mambo mengine kamati hiyo imeadhimia kuwafukuza uanachama Wabunge wake
wanne, ambao ni Anthony Komu, Joseph Selasini, David Silinde pamoja na Wilfred
Lwakatare.
"Ni juu ya madai
yaliyotolewa na Spika kwamba, Wabunge wa CHADEMA waliopewa posho za kujikimu ni
wezi, Kamati Kuu ya chama imelijadili jambo hili na imeamua kwamba madai ya
Spika ni ya uongo na chama kimetoa rai kwa Wabunge kutokutekeleza yale ambayo
Spika ameyaelekeza, ni kinyume na katiba ya nchi, sheria na utaratibu kwani
Wabunge wa CHADEMA siyo wezi" amesema Mnyika.
Aidha
CHADEMA wamesema kuwa watamuandikia barua haraka iwezekanavyo Spika Ndugai, ya
kumjulisha juu ya kuwafuta uanachama Wabunge hao wanne ambao hadi sasa bado
wanaendeleo na vikao vya BUnge.
Mnyika Madai ya Spika ni ya uongo Tumeazimia kama Kamati
Reviewed by KUSAGANEWS
on
May 11, 2020
Rating:

No comments:
Post a Comment