Uchunguzi
wa tukio la kujiua kwa mwanafunzi Faisal Salim (19) wa shule ya Sekondari
Arusha Meru nchini Tanzania aliyejipiga risasi kwa kutumia bunduki ya
baba yake jana Jumapili alfajiri ya saa 11 Agosti 18,2019 unaendelea.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha, Jonathan Shana amesema bado uchunguzi wa tukio hilo unaendelea na hakuna mtu aliyekamatwa.
Katika nyumba aliyokuwa anaishi mtoto huyo na baba yake, Salimu Ibrahimu leo Jumatatu Agosti 19,2019 imefungwa na mmoja wa majirani zake akidai msiba wa mwanafunzi huyo umehamishwa kwa mama yake.
Juma Rashid ambayue ni jirani alisema mwanafunzi huyo amezikwa jana Jumapili katika makaburi ya Njiro jijini Arusha nchini Tanzania.
"Huyu mtoto alikuwa anaishi na baba yake tu, baada ya baba yake katengana na mama yake" amesema Rashid
Jitihada za kumpata baba mzazi wa mwanafunzi huyo bado zinaendelea.
Uchunguzi kujipiga risasi mwanafunzi Arusha unaendelea
Reviewed by KUSAGANEWS
on
August 19, 2019
Rating:
Reviewed by KUSAGANEWS
on
August 19, 2019
Rating:


No comments:
Post a Comment