Kaimu Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Mkoa wa Mara, Dk Hosea Bisanda amezungumzia kifo cha Kasobi Shida (26) ambaye ni mtoto wa dereva wa Mkuu wa Mkoa wa Mara, Adam Malima amesema hali ya Kasobi ilibadilika jana mchana Jumatatu na ilipofika saa 2 usiku mgonjwa huyo akafariki dunia.
Kasobi alilazwa hospitalini hapo Jumapili Agosti 4, 2019 baada ya kupata ajali wakati akiendesha gari linalotumiwa na baba yake, Shida Masaba (55) kumwendesha Mkuu wa Mkoa.
Akizungumza na Mwananchi leo Jumatatu Agosti 6, 2019, Dk Bisanda amesema Kasobi (26) alipokelewa hospitalini hapo Agosti 4,2019 saa 5 asubuhi huku akiwa na maumivu sehemu za tumboni, kifuani na mchubuko kwenye kiwiko cha mkono wake wa kulia.
Amesema baada ya kumpokea alipewa matibabu na kwamba hadi jana Jumatatu asubuhi hali yake ilikuwa inaendelea vizuri.
"Mchana hali yake ilibadilika na hivyo jopo la madaktari wa upasuaji likaamua akafanyiwe upasuaji ambao ulifanyika vizuri lakini ghafla tena hali ikabadilika baada ya upasuaji na akafariki dunia usiku wa jana saa 2," amesema Dk Bisanda
Amesema hali ya Shida Masaba ambaye ni baba wa marehemu inaendelea vizuri ingawa bado watu hawajaruhusu watu kumuona kwa maelezo bado anahitaji muda mwingi wa kupumzika kutokana na kulia mara kwa mara kila anapomuona mtu anaye mfahamu.
"Tunafanya utaratibu namna ya kumjulisha juu ya kifo cha kijana wake maana hali yake bado hivyo inabidi tumpe ushauri wa kisaikolojia kabla ya kumpa taarifa hizi mbaya " amesema Dk Bisanda
Daktari asimulia mazingira kifo cha mtoto wa dereva wa RC
Reviewed by KUSAGANEWS
on
August 06, 2019
Rating:
Reviewed by KUSAGANEWS
on
August 06, 2019
Rating:


No comments:
Post a Comment