Takribani watu wanne wameripotiwa kufariki Dunia katika ajali iliyohusisha basi la abiria la 'Arusha Express' lililokuwa likisafiri kutoka jijini Arusha kueleka mkoani Dodoma kupinduka katika wilaya Babati mkoani Manyara.
Kwa mujibu Kamanda wa Polisi mkoa wa Manyara Agustino Senga, ajali hiyo imetokea majira ya asubuhi ambapo taarifa za awali licha ya vifo hivyo vinne mpaka sasa kuna majeruhi 11 na kati yao watano wako mahututi huku chanzo cha ajali kikiwa bado hakijajulikana.
"Nitatoa taarifa kamili nikiwa nimetulia, mpaka dakika hii vifo ni vinne watatu wamefariki eneo la tukio, na mmoja amefariki hospitali na majeruhi wapo 11 japo hatujajua chanzo cha ajali lakini ajali imetokea upande wenye kona kali na basi likalala upande wa kushoto''. Amesema Kamanda Agustino
Aidha Kamanda huyo amesema bado jeshi hilo linaendelea na shughuli za kufuatilia majina ya wanaotajwa kupoteza maisha kwenye ajali hiyo ili waweze kutambuliwa na ndugu zao.
Basi la Arusha Express Lapinduka....Wanne Wapoteza Maisha
Reviewed by KUSAGANEWS
on
October 08, 2018
Rating:
Reviewed by KUSAGANEWS
on
October 08, 2018
Rating:


No comments:
Post a Comment