Makada 44 wa CCM wamejitokeza kuwania ubunge jimbo la
Korogwe Vijijini.
Makada 47 walichukua fomu hizo na 44 kati yao akiwamo mtoto
wa aliyekuwa mbunge wa jimbo hilo, Thomas Ngonyani wamerudisha leo Agosti 7
Jimbo hilo lilikuwa likiongozwa na Stephen Ngonyani maarufu
Profesa Majimarefu aliyefariki dunia Julai, mwaka huu
Katibu wa CCM Wilaya ya Korogwe Vijijini, Suraisa Sangusa
amezungumza na Mwananchi leo Agosti 7 kuwa, hadi leo saa 12 jioni tayari makada
44 walikuwa wameshawasilisha na fomu kupokewa rasmi.
Amesema kazi iliyobaki ni kwa kamati ya siasa ya wilaya hiyo
kuendesha mchakato wa kuchambua kama waliorejesha wamefuata taratibu zote kabla
ya kuyapeleka majina hayo katika ngazi ya mkoa kwa ajili ya hatua ya awali ya
mchujo
Hata hivyo, katibu huyo amesema majina ya waliorejesha fomu
na kupokewa atayataja kesho
“Naomba ifahamike kwamba hawa waliorejesha fomu wataingia
katika mchujo wa ngazi ya wilaya, mkoa hadi Taifa ili aweze kupatikana atakayeaminiwa
na chama chetu kupeperusha bendera ya kuliwania jimbo hili dhidi ya vyama
vingine,”amesema Suraisa
Jimbo la Korogwe Vijijini limebaki wazi baada ya aliyekuwa
mbunge wake Stephen Ngonyani kufariki dunia mwezi uliopita na jana, Tume
ya Taifa ya Uchaguzi ililitangaza rasmi kuwa wazi na kuruhusu vyama vya
siasa kuendesha mchakato wa kuwateua wanachama wake kuligombea
Makada 44 CCM wachukua fomu kumrithi Majimarefu Korogwe Vijijini
Reviewed by KUSAGANEWS
on
August 07, 2018
Rating:
No comments:
Post a Comment