Baraza la Sanaa la Taifa (Basata), limesema halijawaita wala
kufungia wimbo wa Parapanda uliombwa na wasanii wa kundi la Rostam, Roma
Mkatoliki na Stamina na kusema kuwa labda wameamua kujifungia wenyewe kwa lengo
la kutafuta ‘kiki’.
Kauli hiyo inakuja ikiwa ni siku moja baada ya Roma kupitia
ukurasa wake wa Instagram kuandika maneno ya kuilaumu Basata kwamba inaua vipaji
na ubunifu wa wasanii na kuhoji wimbo wao huo una tatizo gani
Mbali na kuandika hayo pia alizungumza na baadhi ya vyombo
vya habari na kudai kuwa amepewa wito wa kufika Basata
Akilizungumzia hilo, Katibu wa Baraza la Sanaa, Godfrey
Mngereza, amesema hawajaufungia wimbo huo na haujapitishwa mikononi mwao hadi
sasa kwa ajili ya kuhaririwa
"Labda kama wameamua kujifungia wenyewe ili kuufanya
wimbo wao ujulikane na watu, lakini sisi hata hatujauona na kuupitia kama
taratibu zetu zinavyotaka na mnajua tukifungia wimbo huwa tunatangaza sasa
labda Roma awaonyeshe wapi tumesema hivyo," amesema Mngereza
Wasanii hao, Agosti 2 waliachia wimbo huo Parapanda,
unaoelezea masuala mbalimbali yanayoendelea nchini yakiwemo ya kisiasa,
kiuchumi na kijamii
Wimbo huo ambao umeachiwa sauti tu (audio) katika mtandao wa
YouTube, umesindikizwa na picha za hayati Baba wa Taifa Mwalimu Nyerere na
aliyekuwa mwanasiasa mkongwe marehemu Kingunge Ngombare Mwiru
Hata hivyo, katibu huyo alikiri kuwa juzi wasanii hao wawili
kufika katika ofisi za Basata kwa ajili ya kushiriki jukwaa la wasanii ambalo
hufanyika kila siku ya Jumatatu katika ukumbi wao uliopo Ilala Gereji huku mada
kuu kwa siku hiyo ilikuwa kuhusu kanuni mpya za sanaa zilizoanza kutumika Julai
mwaka huu
Katika jukwaa hilo anasema mmoja wa waandishi aliuliza swali
kuhusu matumizi ya picha za waasisi wa mbalimbali wa nchi hii katika
sanaa, ambapo Mngereza anadai alimjibu kuwa msanii anapaswa kupata kibali
kutoka kwa familia au Serikali
"Huenda majibu haya labda ndiyo yalimfanya Roma
akaondoka pale na tafsiri yake na kuandika hicho alichokiandika, lakini
kiukweli hatujamfungia wala kumuita kumuhoji kuhusiana na wimbo hiyo,"
amesema Katibu huyo
Basata yakanusha kumhoji Roma kuhusu Parapanda
Reviewed by KUSAGANEWS
on
August 07, 2018
Rating:
No comments:
Post a Comment